![]() |
|
Rais wa SMZ Dkt Ali Mohamed
Sheid akichuma
karafuu zao maarufu la biashara
visiwani Zainzibar
|
Na Masanja Mabula –Pemba
Migogoro ya ardhi inayoyahusu mashamba ya eka katika Mkoa wa Kaskazini
Pemba inadaiwa kuchangiwa na mmoja wa viongozi wa juu mwenye dhamana kubwa
ndani ya Wizara ya Sheria na Katiba Visiwani hapa .
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwepo na kiongozi
mwenye dhamana katika wizara hiyo ambaye ametoa barua za kuwataka wananchi
waliokabidhiwa eka na Serikali kutoyatumia mashamba hayo na kasha kuyarejesha
kwa wanadaiwa kuwa walikuwa wamiliki kabla ya mapinduzi .
Baadhi ya wananchi wa Shehia ya Ukunjwi , Junguni na Limbani katika
Wilaya ya Wete , wako njia panda juu ya matumizi ya mashamba hayo baada
ya kuwekwa mabango na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana na wananchi hao
kutakiwa kutoyatumia mashamba hayo kwa shughuli za uchumi na maendeleo .
Mmoja wa wananchi Mkaazi wa Ukunjwi Ramadhaman Ali Ramadhan
amesema kuwa kiongozi huyo amemwandikia barua na kusitisha matumizi ya
shamba hilo ambalo amerithi kisheria kutoka kwa mzazi wake ambaye naye
alikabidhiwa na Serikali . lakini Kamisheni imeshindwa kumlipa fidia ya mazao
yake .
“Serikali ya Wilaya na Mkoa pamoja na Wizara ya Ardhi walitaka mimi
niendelee kulitimia shamba hili , lakini baadaye nilipokea bara kutoka kwa
Waziri wa Katiba na Sheria ikinitaka nisitishe matumizi ya shamba hili na mimi
nilidai fidia ya vipando vyangu , kwa mshangao hadi leo sijalipwa ”alifahamisha
.
“Baada ya kupokea barua hii shamba langu limewekwa mabango na kamisheni
ya Wakfu na kuanzia siku hiyo mashamba mengine ambayo nilikuwa nimepekana nayo
pia yamechukuliwa , Je , hii ndiyo azma ya Mapinduzi ? ”alihoji mwananchi huyo
.
Naye Soud Abdalla Mkaazi wa Shehia ya Junguni amesema kuwa Kamisheni ya
Wakfu imewekwa mabango yake kwenye shamba ambalo amelinunua baada ya kustaafu
kazi , na anashangaa kuona kunajitokeza hali hiyo .
“Nilishangaa kuona mabango ya Kamisheni katika shamba langu ambalo
nimelinunua kwa fedha zangui baada ya kustaafu kazi , lakini baada ya hapo
sijaona mtu kudai shamba hilo kwa ni lake na mimi nasubiri atakaye
chomoza na hapo kitaeleweka ”alisisitiza Soud .
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman
amekiri kuwepo na hali ya kuwekwa mabango katika mashamba ya eka pamoja na
maeneo ambayo wananchi wamepimiwa viwanja na Serikali na kudai kuwa hiyi ni
njama ambayo imeandaliwa na kamwe hatakubaliana nayo .
Amesema kuwa wananchi waliokabidhiwa mashamba ya eka na Serikali baada
ya Mapinduzi wanapaswa kuyatunza na kuyaendeleza kwa kupanda miti ya matunda na
biashara ikiwemo mikarafuu na kwamba Serikali haijatoa tamko la kuwaponya
mashamba hayo .
“Mwenye mamlaka na uwezo wa kutengua matumizi ya mashamba hayo ni Rais
wa Zanzibar , hivyo nawaomba wananchi kuyatunza na kuyaendelea mashamba hayo
kwani Serikali bado inatambua umiliki wao kuwa ni halali ”alifahamisha .
Kitendo cha Kamisheni ya Wakfu kuweka mabango katika Mashamba hayo
ambayo yalikabidhiwa wananchi baada ya mapinduzi ya januari 12, 1964
kinakinzana na azma ya mwasisi wa Mapanduzi hayo mzee Abeid Aman Karume
ya kutoa eka tatu tatu kwa wananchi wa Zanzibar .

No comments:
Post a Comment