WATUMISHI wa Mungu
nchini wametakiwa kuhubiri na neno la Mungu wakiwa madhabahuni pamoja kutenga
muda wa kuandaa ujumbe wa neno kabla ya kuhubiri mbele ya waumini
Hali hiyo itawaepusha kuhubiri maneno ya siasa, ndoto zao na
yaliyotokana na mawazo yao.Hayo ameyasema Askofu wa Kanisa la (FPCT) Free Pentekoste Church Of
Tanzania jijini Tanga Askofu Stevie Mulenga ambaye pia anachunga kanisa la FPCT
Novelty, wakati akihubiri katika ibada ya jumapili iiliyofanyika katika kanisa
hilo lililopo Novelty barabara ya nne mjini hapa.
Amesema watumishi walio wengi siku hizi hawapati muda mzuri wa kuandaa
neno au ujumbe na badala yake wanahubiri yaliyopo katika mawazo yao jambo
ambalo ni hatari kwa maisha ya kiroho hususani kwa wale anao walisha.
Akinukuu neon kutoka kitabu cha 1Samweli 1:2,3, Yeremia 23:21-28, Amosi
8:11 na kitabu cha Yohana 1:1-3 Amesema watumishi wanatakiwa kuepuka kusimama
madhabahuni kwa mazoea na badala yake wasimame wakihubiri kile ambacho Mungu
amewaagiza ili kuokoa mioyo za watu ambao Mungu amewapa lakini pia kuishi
maisha yenye ushuhuda mbele za Mungu na mbele za wanadamu.

No comments:
Post a Comment