RATIBA ya mechi za kufuzu michuano ya Mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wa ndani-CHAN inatarajiwa kupangwa Aprili 5 mwaka huu
jijini Cairo, Misri. Timu zipatazo 42 zinatarajiwa kuwemo katika ratiba hiyo
iliyogawanyishwa kwa kanda kutoka mataifa wanachama wa Shirikisho la Soka la
Afrika-CAF.
Kanda ya
Kaskazini ambayo itajumuisha timu za Libya, Morocco na Tunisia watacheza
wenyewe katika hatua ya mzunguko huku timu mbili za juu zikitarajiwa kufuzu kwa
ajili ya fainali hizo.
Kanda
zingine zitakuwa zimegawanywa kama ifuatavyo, kanda ya magharibi A itakuwa na
timu za Gambia, Guinea, Guinea Bissau, Liberia, Mali, Mauritania, Senegal,
Sierra Leone ambapo washindi wawili ndio watasonga mbele.
Magharibi
B kutakuwa na Burkina Faso, Côte d’Ivoire, Ghana, Niger, Nigeria, Togo ambapo
pia timu mbili ndio zitasonga mbele huku kanda ya kati ikijumuisha timu za
Cameroon, Afrika ya Kati, Congo, Chad, DR Congo, Gabon na timu tatu ndio
zitasonga mbele.
Kanda ya
kati-mashariki itakuwa na timu za Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Sudan,
Tanzania, Uganda ambapo timu tatu pia ndio zitasonga mbele huku kanda ya Kusini
ikijumuisha timu za Angola, Botswana, Comoros, Mauritius, Lesotho, Mozambique,
Namibia, Seychelles, South Africa, Swaziland, Zambia and Zimbabwe.
Mechi za
kufuzu zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Juni 19 mpaka 21 na Agosti 28
mpaka 30 ambapo timu 15 zitakazofuzu zitaungana na wenyeji Rwanda katika
fainali ya michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Januari 16 mpaka Februari 7
mwakani.
No comments:
Post a Comment