Wafanyabiashara
wa
gulio la Tangamano wameilalamikia serikali juu ya suala zima la uchafu
uliokithiri katika gulio hilo na kuwahatarisha afya zao .
Akizungumza
na Redio Huruma akiwa gulioni hapo katibu wa Gulio Proti Mramba amesema kwamba
kutokana na ongezeko la wafanya biashara katika gulio hilo imekuwa ni chanzo
kikubwa kwa uchafuzi wa Mazingira ya gulio .
Hivyo
ameiomba Halmashauri ya Jiji iliangalie suala
hilo kwa jicho la tatu kwa kuwapatia Skip ya kuwekea takataka hizo ili kuweka afya ya wananchi
salama.
Hata
hivyo mmoja wawafanya biashara hao
Cyprian Joseph Mmassy amesema kuwa serikali imekuwa wazito sana kuwapa
kipaumbele wafanyabiashara wadogo wadogo hali ya kuwa na wao kuwa wanamchango
mkubwa katika maendeleo ya jiji.
Pia
ameishauri serikali iwaboreshee miundo mbinu ya Gulio hilo hususan choo na mabanda
ya kudumu ya kufanyia biashara zao.
Naye
afisa afya wa jiji Kizito Nkwabi amesema kuwa eneo la gulio halina sababu ya
kuwapelekea skip kwani viongozi wa gulio kwa kushirikiana wafanyabiashara
wanajukumu la kuondoa takataka hizo.
Kwa
uapande wake mkurugenzi wa jiji la Tanga Wilfred Lazaro amesema kuwa hakuna
sababu ya kuwajengea mabanda ya kudumu kwani eneo hilo sio rasmi bali ni la
muda mfupi kwa wafanyabiashara hao.
Sambamba
na hayo amesema kuwa halmashauri imetenga eneo la maalumu la kudumu kwa gulio
kwa ajili ya wafanyabiashara wa jiji la Tanga ambalo lipo maeneo ya Muhako
jijini hapa.
No comments:
Post a Comment