Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya makaravati yaliyowekwa kwenye barabara ya Kigombe-Mtiti Wilayani Muheza yamebainika kutengenezwa chini ya kiwango na kuwekwa barabarani bila kuwa na vyuma(Nondo) ambazo huzuwia magari yenye uzito mkuwa yasifanye uharibifu.
Mwandishi
wa Mtandao huu Godwin Henry(Pichani) ameshuhudia makaravati mawili katika barabarani
hiyo yakiwa yamebomoka kwa kushindwa kuhimili uzito uliopita juu yake. Bara
bara hiyo imefanyiwa ukarabati wiki chache zilizopita na kugharimu pesa za
walipa kodi wa Tanzania kwa kumlipa mkandarasi huyo.
Wakizungumza
na Mtandao huu baadhi ya watumiaji wa Barabara hiyo wameezwa kusikitisha kwao
na ukarabati huo ambao umefanyika chini ya kiwango.
Wamesema
kubomoka kwa makaravati hayo kunahatarisha usalama wa watumiaji wa barabara
hiyo hasa wanaopita usiku na wanaotoa mazao mashambani kwa Malori kwani
yanaweza kukwama kwenye makaravati hayo.
No comments:
Post a Comment