Wanafunzi wa Shele ya Msingi Mtiti |
Kamati ya udhamini wa Vifaa vya Michezo wilayani
Muheza(Muheza Players Committee) imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa shule
ya msingi Mtiti iliyoko kata ya Kogombe wilayani Muheza kwa lengo la kuinua ari
ya michezo na vipaji vya wanafunzi Shuleni hapo.
Mratibu wa Kamati hiyo Athumani Mtoro (Kushoto, mwenye shati la Njano) akikabidhi msaada huo kwa Mwalimu wa Michezo Shuleni hapo.
Baadhi ya Timu za Netball za Wanawake zilizo nufaika na Misaada ya Kamati hiyo. |
Vifaa hiyo ni Mpira wa Netball,miamba miwili ya
kuchezea Basket ball na mfuko mmoja wa saruji.Akikabidhi msaada huo Mratibu wa
kamati hiyo Bw.Athumani Mtoro amesema kamati hiyo imejipanga kuziwezesha shule
nyingi zaidi kupata vifaa vyote muhimu kwa ajili ya michezo ili kuinua vipaji
wilayani humo.
Amesema mpaka sasa tayari shule nyingi za Msingi
na Sekondari ambazo zinamilikiwa na Serikali wilayani humo zimenufaika na
mpango huo ambao unalenga hasa wanafunzi wa Kike ambao wamesahaulika katika
Michezo.
Akipokea msada huo Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mw.
Sadiq Kalage ameishukuru kamati hiyo na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo ili
wanafunzi wengi zaidi wanufaike navyo.Amesema kupatikana kwa vifaa hivyo
kutasaidia kujenga Afya za wanafunzi hao na kutokomeza tatizo la Utoro wa
wanafunzi kwani wengi wao wanapenda sana michezo.
Naye Msimamizi wa Kamati hiyo Bw Salim Salehe wa A
& G STATIONARY ya Kigimbe Malaki amesema ni wamepokea changamoto nyingine
za kimichezo shuleni hapo kama na Mpira wa Miguu, Filimbi, Jezi, Viatu vya
michezo na kuahidi kuzitatua kwa kipindi kisicho zidi Miezi Miwili.
No comments:
Post a Comment