Christiano Ronaldo |
Klabu ya Manchester United imeanzisha mazungumzo
na ajenti wa Christiano Ronaldo kwa lengo la kumrudisha Old Trafford.
Siku za usoni
za Ronaldo zimejaa uvumi huku kukiwa na madai kwamba mchezaji huyo hafurahii
maisha ya Madrid.
Wakala Jorge Mendes |
Habari hizo
zimeifungua macho United na sasa ripoti nchini Uhispania zinasema kuwa
Manchester United imeanzisha mazungumzo na ajenti wa mchezaji huyo Jorge Mendes
kwa lengo la kumrudisha mchezaji huyo Old Trafford.
Kulingana na
gazeti la Metro nchini Uingereza United ina matumaini ya kumpata Ronaldo kwa
kitita cha yuro millioni 100 ambazo ni sawa na pauni millioni 71.1.
Haijulikani
iwapo raia huyo wa Ureno atakubali kurudi Manchester United ,licha ya kuipenda
kilabu hiyo.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment