HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 14 March 2015

LIGI KUU TANZANIA BARA "OKWI HATARIII AWAKAANGA MTIBWA DAKIKA ZA MAJERUHI"



Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba SC toka Uganda Emanuel Okwi amedhihirisha ubora wake na leo tena baada ya kuipatia timu yake ya Simba SC goli pekee la ushindi mbele ya ya wakata miwa wa Mtibwa sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom Mtibwa sugar waliuwanza vyema mchezo kwa kucheza kwa uwelewano zaidi katika kipindi cha kwanza ambapo Simba SC walikuwa wakichezea mpira zaidi katika eneo lao.

Katika kipindi hicho cha kwanza ambapo Mtibwa sugar walifika langoni mwa Simba SC mara nyingi zaidi, Simba SC walikuwa wakitumia mipira mirefu, wakitaka kutumia udhaifu wa beki ya mtibwa sugar ya kutokuwa na mbio lakini kipa wa Mtibwa sugar alikuwa akiiwahi mipira yote mirefu iliyokuwa ikielekezwa kwa Okwi na Saimon Sernkuma.

Kipnid cha pili hali ilikuwa tofauti, kwani simba sc walirejea na mipango mingine tofauti na ile ya awali, mara baada ya Ramadha Singano kuingia kuchukuwa nafasi ya Sernkuma.

Kocha wa Mtibwa sugar huenda akajilaumu kwa mabadiliko aliyo yafanya ya kumpumzisha Mussa Mgosi ambate aliwapa wakati mgumu Simba SC kwa takribani dakika 75 alizocheza na nafasi yake ikachukuliwa na Vicent Barnanbas.

Mabadilok ya kumtoa Mgosi yalipelekea Simba SC kulisakama lango la Mtibwa sugar na kupelekea Mtibwa sugar kuwa na waktai mgumu katika dakika 15 za mwisho wa mchezo.

Katika dakika za nyongeza Emanuel Okwi alipiga shuti mbele ya beki Saidi Mkopi na Henry Joseph, na shuti hilo kutinga katika nyavu za Mtibwa sugar na kupaitia Simba SC pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa leo.

MATOKEO YA MICHEZO MINGINE YA LEO
SOKOINE -MBEYA
Prison 3-0 Stand United

JAMHURI-MOROGORO
Polisi Moro0-1 JKT Ruvu

MABATINI -PWANI
Ruvu Shooting 1-1 Coastal Union

No comments:

Post a Comment