Mkuu wa mkoa wa Tanga
Magalula Saidi Magalula
|
UTORO umetajwa kuwa changamoto kubwa katika sekta ya
elimu mkoani Tanga hali inayosababisha wanafunzi wengi kukatisha masomo yao ya
msingi na sekondari.
Akiongea katika kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa RCC
Mkuu wa mkoa wa Tanga Magalula Saidi Magalula amesema kwa kipindi cha miaka
saba hadi 2014 zaidi ya wanafunzi 13,000 wameacha shule kwa sababu mbalimbali
ikiwemo utoro na mimba.
Amesema wanafunzi wengi waliofaulu kwenda kidato
cha kwanza mwaka 2015 bado hawajaenda shule na kuwaagiza wakurugenzi wa
Halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha hakuna mtoto yeyote atakayerudishwa
kwa uzembe wa mzazi wake kukosa ada.
Aidha amesema Mkoa bado unakabiliwa na changamoto
kubwa za kielimu ikiwemo uhaba wa miundombinu ya madawati, vyumba vya madarasa
na matundu ya vyoo.
No comments:
Post a Comment