MTU mmoja aliyefahamu kwa jina la Bakari Nyoka anayekadiriwa kuwa na umri
wa miaka kati ya 25 hadi 30 mkazi wa Magomeni ameuwawa na wananchi wenye hasira
kali baada ya kutuhumiwa kuiba pikipiki.
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo Kaimu kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Tanga Juma Ndaki
amesema tukio hilo limetokea manamo tarehe 12 march mwaka huu majira ya saa
kumi kamili jioni huko katika maeneo ya kijiji cha kilapura tarafa ya pongwe wilaya ya Tanga.
Aidha Ndaki amesema Marehemu
aliuwawa baada ya kutuhumiwa kuiba pikipiki yenye namba za usajili T.833 BFQ
aina ya belter ambayo ni mali ya mkulima Stevene Alexander mwenye umri wa miaka
40 mkazi wa michungwani wilayani Handeni.
Hata hivyo amesema
hakuna mtu au watu waliokamatwa na
upelelezi wa tukio hilo unaendelea dhidi ya wahusika wa mauaji hayo, na
mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
hospitali ya rufaa ya mkoa Bombo.
No comments:
Post a Comment