HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 11 March 2015

"BONYEZA HAPA" KUONA MKUSANYIKO WA PICHA ZA AJALI ILIYOUA WATU 42 NA KUJERUHI 22 MKOANI IRINGA LEO.






Majeruhi wa Ajali hiyo wakiwa Hospitali kwa matibabu



Shimo lililokuwa linakwepwa na Madereva wa Magari hayo na kusababisha ajali
Zoezi la kuwaondoa majeruhi eneo la tukio likiendelea

HAYA NI MATUKIO YA KUSISIMUA KUHUSU AJALI HIYO.


MAAJABU na kweli moto  wa  miaka 3 asalimika kwa  kutokuwa na mchubuko  wowote baada ya ajali   basi la kampuni ya majinja  lenye namba  za usajili T 438 CDE aina ya  Scania  lililoua  watu  42  na  kujeruhi 22 kufuatia  basi hilo  kutoka Mbeya  kwenda  Dar es Salaam ugongana uso kwa Uso na Lori na  kufunikwa na kontena la  lori  hilo.

Katika  ajali  hiyo  imeelezwa  kuwa  mtoto  huyo ambae  jina lake  halijafahamika  alikuwa akisafiri na  wazazi  wake  wote  wawili  kutokea  Mbeya  kwenda  Dar es Salaam na  baada ya ajali  hiyo mtoto  huyo  alichomoka katika mikono ya  mzazi  wake na kukutwa chini ya siti nyuma na basi hilo ambako hakukuharibika  kabisa.

Mmoja kati ya  abiria  wa  ajali  hiyo  Lucy Mtanga amesema mtoto  huyo alikuwa amekaa siti  za mbele  kama  siti ya  tatu kutoka kwa  Dereva  pamoja na  wazazi   wake na cha ajabu baada ya ajali  hiyo mtoto  huyo alikutwa  chini ya  siti ya  mwisho kabisa mwa basi hilo akiwa ametulia.

Katika  ajali  hiyo  iliyotokea  leo   Majira ya saa 4 asubuhi eneo la Changalawe nje kidogo ya Mjini wa mafinga wilaya ya Mufindi mkoani  hapa katika barabara kuu ya Iringa - Mbeya abiria  wake  waliopoteza maisha  walisagika  vibaya kichwani na wengi  wao miguu  kuvunjika vunjika  huku  sura  zao  zikishindwa  kutambulika .

Imeelezwa pia katika  basi hilo kulikuwa na baadhi ya  wanafunzi  kutoka   shule ya  sekondari  Sangu  mkoani Mbeya  akiwemo ndugu  wa Mwanahabari na meneja  wa  gazeti  la Mtanzania  mkoani Iringa Marcy Mwalusamba  kijana   Omega  Mwakasege  aliyekuwa akisoma  shule ya  sekondari  Sangu  ambae alifariki wakati akipatiwa matibabu  katika  Hospitali ya wilaya ya  Mufindi ..

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa jumla ya watu 41 walikufa eneo la tukio na mmoja alifia hospitali ya wilaya ya Mufindi na mmoja kufariki akiwa anapatiwa matibabu hospitalini hapo.

Pia alisema watu 22 akiwemo Mtoto wa miaka mitatu wamejeruhiwa vibaya huku zaidi ya 10 hali zao ni mbaya zaidi.

Mkuu huyo wa Mkoa pia aliagiza maiti 32 kupelekwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Baada ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo ya wilaya ya Mufindi kutokuwa na uwezo wa kuhifadhi miili zaidi ya 8.

Wakati  mkuu  wa mkoa wa Iringa  akitaka  chanzo  cha ajali  hiyo  kuchungwa  zaidi baadhi ya majeruhi  wa ajali  hiyo wameibuka na kusema  kuwa  chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na mashimo makubwa yaliyokuwepo Eneo hilo.

JOsamu Obedi alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa katika mwendo mkali toka anatoka Eneo la Uyole Mbeya na kufanikiwa kuyapita mabasi zaidi matano yaliyokuwa yameondoka stendi ya Mbeya mjini saa 12: 00 asubuhi .

Hata hivyo Kabla ya kufika Eneo la ajali zaidi ya mara tatu abiria walimuonya kupunguza mwendo japo hakusikiliza zaidi ya kuwakejeli kuwa yeye ni zaidi ya dereva hivyo wasimfundishe kazi.

Pia alisema kuwa basi hilo hilijaza abiria na baadhi yao kukaa nyuma ya dereva kwa kutandikiwa godoro na  kuwa mwendo kweli ulikuwa mkali zaidi na ndio maana uwezekano wa kukwepa mashimo ulikuwa mdogo  hivyo  kusababisha ajali  hiyo .

Alisema Baada ya kufika eneo hilo lenye mashimo makubwa barabarani kushoto na kulia lori lilitaka kupita katikati na basi pia lilitaka kupita ebeo hilo ndipo yalipokutana uso kwa uso.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Iringa Salim Asas akizungumza Eneo la tukio mbali ya kuwapa pole ndugu wote waliopoteza Maisha ,alisema kuwa ajali hiyo ni kubwa kwa Mkoa wa Iringa na haijapata kutokea ajali Kama hiyo toka ameingia mwaka 2008 hajapata kushuhudia ajali mbaya Kama hiyo.

Alisema kuwa Mkoa wa Iringa umekuwa ukisifika kwa kutokuwa na ajali mbaya na kuwa mwaka Jana umepewa tuzo ya kitaifa ya kuongoza bila ajali kubwa.

Hivyo alisema kwa tukio hili kuna haja ya kujitathimini na kuangalia sababu ya ajali hiyo ambayo wapo wanaosema ni mashimo barabarani na wapo wanaosema mwendokasi wa madereva.

Alisema eneo hili lina mteremko mkali na mlima na kuwa lori lilikuwa likishuka na basi lilikuwa linajiandaa kupanda mlima baada ya kushuka mteremko kwa kasi .

Hivyo alisema iwapo sababu kubwa ni mashimo basi wahusika kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo huku akiwataka madereva pia kuwa makini zaidi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo mbaya na kuwa uchunguzi zaidi unaendelea.

Kuhusu hali za madereva kamanda Mungi alisema hana uhakika Kama wamepona ama wamekufa kutokana na miili yao kuharibika zaidi na wapo ambao ni mahututi .

 Wakati ajali  hiyo ya  kihistoria  ikitokea  mkoani  Iringa katika  wilaya ya  Mufindi taarifa   kutoka katika  wilaya  hiyo  zinadai  kuwa mkuu  wa wilaya ya  Mufindi  Bi  Mboni Mhita  ndio  ilikuwa ni  siku yake ya  kwanza ya  kuanza kazi rasmi  katika  wilaya  hiyo baada ya  kuapishwa na kurudi kwao kuchukua mizigo  yake.

Mkuu  huyo  wa  wilaya  ambae  hakutaka  kuzungumza  chochote na wanahabari alionekana ni mwenye  mawazo na asiyejua nini  cha  kufanya kufuatia tukio  hilo pamoja na  kuvaa gropsi mikononi kwa ajili ya  kusaidia kupakia  majeruhi na maiti  ila hakuweza  kufanya  hivyo

Wakati  huo  huo  wananchi  wenye  hasira kali  walishindwa  kujizuia  kumtolea  lugha kali na  kumzonga  mkuu  wa mkoa  wa Iringa pamoja na .kamati ya  ulinzi na usalama  ya mkoa  wakilalamikia mashimo  hayo kuwa  ajali  hiyo ni uzembe wa  serikali  kupitia  TANROADS kutokana na mara kwa mara  madereva  kulalamikia mashimo  hayo kwa  zaidi ya mwaka  sasa  bila  kutengenezwa .

Mbali ya  tukio  hilo kijana mmoja ambae  jina lake  halikufahamika  mara  moja  alinusurika  kichapo  na  kuishia  kuvunjiwa simu yake aina ya Nokia kutoka kwa  wanajeshi wa JKT Mafinga  ambao  walifika  kusaidia  ulinzi na uokoaji  eneo hilo kwa  kile walichoeleza ni  kumpiga  picha mmoja kati ya wanajeshi hao  wakati akimthibiti kibaka aliyekuwa akitaka  kupora mali za marehemu bila  ridhaa yake.

VYANZO: IRINGA YETU.
FRANCIS GODWIN.

No comments:

Post a Comment