Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
wa Manyara imetembelea katika migodi iliyoteketea kwa moto katika machimbo ya
Tanzanite Mirereani Simanjiro huku mkuu wa mkoa huo Joel Bendera akiwaagiza
wataalam wa Tanesco idara ya madini na jeshi la polisi kufanya uchunguzi
wa haraka kugundua chanzo cha moto huo ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa
watakao bainika.
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa
aliongozana na wataalam wa Tanesco idara ya madini na vyombo vya ulinzi na
usalama ambapo kabla ya kuzungumza na wananchi alitoa nafasi kwa waathirika
kutoa madukuduku yao nawo waliendelea kulalamikia uzembe uliyofanyika katika
tukio ilo na kuendelea kusisitiza kuwa kuna hujuma katika tukio ilo na wengine
wakilalamikia njaa na mazingira magumu ya kulala.
Akitoa maelezo ya awali mkuu wa
wilaya ya Simanjiro Mahamud Kambona ameeleza namna tukio ilo lilivyo waathiri
wachimbaji wadogo na hatua za awali walizochukua.
Ukafika wakati wa mkuu wa mkoa wa
Manyara Dk Joel Bendera kutoa pole kwa niaba ya serikali na kuviagiza vyombo
vinavyo husika kufanya uchunguzi wa kina kwa haraka ili kujuwa kama ilikuwa ni
ajali ya kawaida au ni hujuma huku mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara
Christopher Fuime akitoa angalizo kwa wachimbaji wadogo kuhusu uhifadhi na
matumizi ya mulipuko.
No comments:
Post a Comment