Jeshi la wananchi wa Tanzania limewaondoa hofu watanzania
kuhusu tishio la matukio ya kigaidi na kuongeza kuwa jeshi hilo liko imara
kukabiliana na hatari yeyote huku mahusiano baina ya Tanzania na Malawi
yakielezwa kuwa imara na ya kindugu kufuatia ziara ya kikazi ya mkuu wa majeshi
ya Malawi kuzuru hapa nchini kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya majeshi ya
Tanzania na Malawi.
Mkuu wa majeshi ya Malawi jenerali
Ignacio Maulana mara baada ya kuwasili katika viwanja vya makao makuu ya jeshi
yaliyoko Upanga jijini Dar es Salaam amepata heshima ya kukagua gwaride maalum
lililoandaliwa kwa ajili yake na mwenyeji wake jeneral Davis Mwamunyange na
kisha kupata fursa ya kufanya mazungumzo ya faragha.
Mara baada ya mazungumzo ya faragha
baina ya wakuu hao wa majeshi ya Tanzania na Malawi wamejitokeza mbele ya
waandishi wa habari ambapo mkuu wa majeshi ya Tanzania jenerali Davis
Mwamunyange amezungumzia pia suala la matishio ya kigaidi hapa nchini na
kuwaondoa hofu watanzania kwakusema jeshi hilo liko imara.
Kwa pamoja wakizungumzia mahususiano
baina ya nchi hizo wakuu hao wa majeshi wamesema uhusiano ni imara ambapo
viongozi wakuu wa kitaifa pamoja na wale wa kijeshi wanapata fursa ya
kutembeleana huku mkuu wa majeshi ya Malawi akisema kuwa mahusiano baina ya
nchi hizo hayawezi kuchukuliwa kimzaha kwa kuwa ni ya kihistoria.
Mara baada ya mazungumzo hayo wakuu
hao wa majeshi wameelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuonana na
rais.
No comments:
Post a Comment