Mkuu wa
Wilaya ya Micheweni
Bw Jabu
Khamis Mbwana
|
Na Masanja Mabula Pemba.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni bw Jabu Khamis
Mbwana amewataka vijana wanaopewa dhamana ya ulinzi na wawekezaji katika maeneo
ya mahoteli kutojihusisha na masuala ambayo yanaweza kupelekea migogoro kwa
wananchi.
Kauli hiyo ameitowa huko Ofisini kwake Micheweni wakati akizungumzia migogoro ya ardhi inayo endelea kutokea siku hadi siku katika shehia ya Makangale.
Amesema ni vyema wawekezaji wanaofika katika maeneo hayo kufuata mila, desturi pamoja na tamaduni za wananchi wa eneo hilo ili waweze kwenda sambamba na kuepusha migogoro isiyo kuwa ya lazima.
Jabu amesema ni vyema wawekezaji kuwa na maelewano mazuri na wananchi wa
maeneo husika kabla ya kufanya ujenzi katika maeneo hayo ili kuepusha migogoro
inayoweza kuepukika
Amesema kuwa mwekezaji huyo alipaswa
kuweka njia mbadala kabla ya kuiziba njia hiyo ya asili inayotumiwa
na wananchi kwa kipindi tangu enzi za Mapinduzi ya january 1964 .
No comments:
Post a Comment