Jana Usiku Barcelona
na Juventus zimekamilisha idadi ya Timu 8 zitakazocheza Robo Fainali ya UEFA
CHAMPIONZ LIGI Mwezi ujao.
Barcelona,
wakiwa wameshinda Mechi ya Kwanza 2-1 huko Etihad, Jana ndani ya Nou Camp
waliifunga Man City Bao 1-0 na kuhakikisha kuwa England, kwa mara ya pili
katika Misimu mitatu, haina Timu kwenye Robo Fainali ya Mashindano haya na pia
kuleta mashaka kwa Meneja Manuel Pellegrini kwenye himaya yake huko City baada
kupokea kipigo cha 4 katika Mechi 5 zilizopita huku wakionekana kushindwa
kutetea Taji lao England wakiwa Nafasi ya Pili na Pointi 6 nyuma ýa Vinara
Chelsea ambao pia wana Mechi 1 mkononi.
City,
ambao wanadaiwa kuwa na Timu inayolipwa vizuri zaidi huko Ulaya, sasa
haijatinga Robo Fainali ya Mashindano haya katika majaribio yake Manne
yaliyopita.
Bao
la Barca hiyo Jana lilifungwa na Rakitic katika Dakika ya 31 baada pasi murua
ya Lionel Messi.
Katika
Mechi nyingine iliyochezwa Jana huko Signal Iduna Park, Wenyeji Borussia
Dortmund walipigwa 3-0 na Juventus na kutupwa nje kwa Jumla ya Bao 5-1 baada ya
kufungwa Mechi ya kwanza 2-1 huko Turin.
Bao
za Juve zilifungwa na Carlos Tevez, Bao 2, na Alvaro Morata.
Barca
na Juve zinaungana na Real Madrid, Mabingwa Watetezi, FC Porto, Bayern Munich,
PSG, Atletico Madrid na AS Monaco kwenye Robo Fainali ambayo Droo yake
itafanyika kesho.
No comments:
Post a Comment