Na.Mwandishi Wetu.KOROGWE
TAASISI
ya Global medical aid yenye makazi yake nchini Denmark imewakabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya tsh million
630 kwa hospitali ya Magunga iliyopo wilayani Korogwe ili kuboresha upatikanaji
wa huduma za matibabu kwa wananchi.
Makabidhiano ya vifaa vya tiba hivyo
yalifanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya NIMR vilivyopo eneo la hospitali
ya Magunga na na mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya Korogwe aliyewakilishwa na
Diwani Idd Shebila.
Kabla ya msaada huo kukabidhiwa Mkurugenzi
wa NIMR mkoani hapa Cletus Ruta amesema vitu vilivyotolewa ina ubora na ili
kudumu kwa muda mrefu iko haja ya kukarabatiwa mara kwa mara.
Vifaa vilivyo kabidhiwa hospilani hapo ni pamoja na
vitanda ,mashine ya ultra, sound, groves na vitu vingine ambavyo
vilipata kuwa pungufu kwenye eneo hilo la utoaji wa huduma za afya.
Akizungumza kwenye hafla hiyo mwakilishi wa
Global medical Aid Dkt. Christentze Schmiegelow amesema mahusiano ya kuenziwa
kati ya NIMR ,Magunga hospitali na chuo kikuu cha Copenhagen cha Denmark ndiyo
yaliyowezesha upatikanaji wa vifaa
hivyo.
Amesema mbali na wao kushghulikia na utafiti
wa magonjwa a ya bianadamu kwa
kushirikiana na kituo cha utafiti NIMR waliwiwa kusaidia vifaa vya tiba ili kuboresha huduma za wananchi wa Korogwe.
Naye idd Shebila ambaye ni mwenyekiti wa
kamati ya huduma za jamii halamashauri aliwataka madaktari kutumia taaluma zao kupitia vifaa
walivyopewa kuboresha afya za wananchi.
Shebila amesema kwamba kupatikana kwa vifaa
hivyo ni ukombozi kwa wananchi wa Korogwe ambapo awali walikuwa wakikabiliwa na
changamoto ya upungufu wa vifaa vya tiba
huku muda wote wakitegemea MSD.
Kwa upande wake mganga mkuu wa hopitali ya
Magunga wilayani korogwe Dkt Olden Ngasa ametoa shukrani kwa msaada
waliyopasiwa huku akitoa ombi kwa
wahisani hao kuangalia uwezekano wa kusaidia eneo jingine hususanii maeneo ya
vijijini.
No comments:
Post a Comment