Na. Masanja Mabula Pemba
Mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba Mhe
Omar Khamis Othman ameagiza taasisi zinazohusika kufanya tathmini ya
vipando vya wananchi katika eneo la vumawimbi makangale ili ujenzi wa mradi wa
hoteli ya kitalii uweze kutekelezwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba
Mhe Omar Khamis Othman
|
Amesema kuwa tathmini hiyo itawawezesha
wananchi kulipwa fidia ya vipando vyao jambo ambalo linatakiwa kufanyika
mapema ili mradi uanze utekelezaji wake.
Kauli hiyo ameitoa wakati
akizungumza na wananchi wa kijijini shehia ya makangale pamoja na mwekezaji
baada ya kumalizika kwa mgogoro wa eneo ambapo pande hizo zimekubaliana
kushirikiana ili kutekeleza dhana ya utalii kwa wote.
Aidha amesema kuwa uwamuzi
uliofikiwa na wananahci wa shehia ya makangale na mwekezaji unapaswa
kuigwa na maeneo mengine yenye migogoro ya ardhi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya
micheweni bw jabu khamis mbwana amesema kuwa makubaliano hayo yamekuja kufuatia
wananchi wa shehia hiyo kufahamu faida na umuhimuwa wa sekta ya utalii.
Katika ziara hiyo pia mkuu wa mkoa
ametembelea maeneo mengine yenye mgogoro wa ardhi likiwemo shamba la mzee ali
said radhaman ambalo linadaiwa kupimwa na kumilikishwa Mhe Samiya Suluh Hassan.
KATIKA HATUA NYINGINE Mkuu wa Wilaya ya
Micheweni bw Jabu Khamis Mbwana ameitaka jamii kuepuka tamaa ya fedha kwa
kuyauza mashamba yao watu zaidi ya mmoja ili kuepusha kutokea kwa migogoro ya
ardhi katika maneo yao .
Amesema kuwa migogoro
mingi ya ardhhi inayojitokeza siku hadi siku inasababishwa na jamii kuwa na
tamaa ya fedha hali ambayo inawafanya kukosa uwaminifu na hivyo kujikuta
wakisababisha kuwepo na migogoro.
Akizungumza na wananchi
wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika shehia
ya Makangale Jimbo la Konde , Mkuu huyo wa Wilaya ameshusha presha za wananchi
hao baada ya kuahidi kuipatia ufumbuzi migogoro hiyo.
Amekiri kuwa shehia ya
Makangale na Tondooni zinakabiliwa na migogoro mingi ya ardhi na kuwataka
wananchi wa shehia hizo kumpa ushirkiano ili aweze kutekeleza azma yake ya
utatuzi wa migogoro kwa lengo la kulinda amani na utulivu uliopo hapa nchini.
Naye Katibu Tawala wa
Wilaya hiyo bw Ahmed Khalid Mohemmed amewataka wawekezaji kuacha kupora ardhi
za wananchi , na badala wawashauri na kuwepo makubaliano ya
pande zote zinazohusika.
Migogoro mingi ya ardhi katika
shehia hizo unahusu wananchi na wawekezaji , viongozi wa serikali na wananchi
pamoja na wananchi wenyewe kwa wenyewe.
No comments:
Post a Comment