Baada ya kufunga mabao yote ya ushindi
wa Yanga SC wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa jijini hapa Jumapili,
Ngasa alidai kuwa Yanga SC imemtelekeza katika kulipa deni la zaidi ya Sh.
milioni 40.
Ngasa, mchezaji wa zamani wa Kagera
Sugar FC, Azam FC na Simba SC ambaye pia amefunga mabao 28 Taifa Stars katika
mechi 80 alizoichezea, aliangukia kwenye deni hilo kubwa kwa hadhi ya wachezaji
wa ndani ya Tanzania baada ya kuamuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
kuilipa Simba SC Sh. milioni 30 na penalti ya asilimia 50 (Sh. milioni 15)
baada ya kupatikana na kosa la kusaini mikataba ya kuzitumikia klabu mbili
msimu mmoja, Simba SC na Yanga SC msimu uliopita.
Ngasa aliyezaliwa Mwanza, pia
alifungiwa mechi sita kutokana na kosa hilo msimu uliopita, lakini akaibuka
mfungaji bora wa Yanga SC na mfungaji bora wa Klabu Bingwa msimu uliopita.
Ngasa alifunga mabao 13 na kutoa pasi
17 za mwisho katika ligi kuu ya Bara licha ya kukosa mechi tano za mwanzo na
ile ya Ngao ya Jamii waliyoshinda dhidi ya Azam FC.
Baada ya kuibuka kwa mvutano kati yake
na uongozi wa Yanga SC kuhusu adhabu hiyo, Ngasa alilazimika kukopa pesa CRDB
kwa udhamini wa klabu hiyo ya Jangwani, lakini Jumapili aliibua mambo makubwa
akidai ametelekezwa na klabu na sasa hachukui hata shilingi moja kutokana na
mshahara.
"Muda wote klabu haijanisaidia
kwa lolote kulipa deni hilo, nimekuwa nikikatwa kila mshahara wangu unapoingia
na sasa hali imekuwa mbaya zaidi maana sasa wanachukua mshahara wote bila
kuniachia chochote," alisema Ngasa katika mahojiano na waandishi wa habari
baada ya mechi ya Jumapili.
Ngassa amekwenda mbli zaidi na kueleza kuwa amekuwa akikatwa mshahara na pesa hizo hazikuwa zikifika benki jambo ambalo linamchanganya sana kwa sasa.
Ngassa amekwenda mbli zaidi na kueleza kuwa amekuwa akikatwa mshahara na pesa hizo hazikuwa zikifika benki jambo ambalo linamchanganya sana kwa sasa.
Hata hivyo, Yanga SC kupitia kwa Mkuu
wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Jerry Muro, imesema Ngasa 'amewewezeshwa' na
furaha ya mabao yake mawili dhidi ya Mtibwa Sugar kiasi cha kuanza kupotoka
mambo ya deni lake na CRDB.
"Yanga SC haidaiwi na Mrisho
Ngasa, lakini kilichopo ni deni la mchezaji kwa benki ya CRDB. Kesho Jumanne
saa 4:30 tutazungumza na waandishi wa habari kwa kina kuhusu suala hilo na
Ngasa mwenyewe atakuwapo kueleza ukweli wake," amesema Muro.
Katika mkutano huo na waandishi wa
habari, Muro amesema wataweka wazi bei ya tiketi a mechi yao ya Jumapili dhidi
ya BDF XI ya Botswana, ikiwa ni mechi ya hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho
barani Afrika mwaka huu.
Soka la Tanzania linakabiliwa na
changamoto ya wachezaji na klabu kutoheshimu mikataba ya wachezaji hususan
kipindi cha usajili, jambo ambalo limekuwa likizigharimu klabu na wachezaji
mamilioni ya shilingi.
No comments:
Post a Comment