Katika mchezo uliopita wa Yanga dhidi ya Mtibwa ligi kuu ya Soka Tz Bara Yanga ilipata ushindi mnono 2-0 dhidi ya timu ngimu msimu huu Mtibwa Sugar huku mabao yote yakifungwa na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa.
Habari kubwa sasa ni kile alichoonesha Ngasa baada ya bao la kwanza kwa mashabiki wa Simba sasa Habari kubwa ni kuwa Uongozi wa klabu hiyo unajipanga kumaliza soo kijanja "hebu fuatilia taarifa hii iliyowekwa kwenye ukurasa wa Wapenzi na Mashabiki wa Yanga."
Habari kubwa sasa ni kile alichoonesha Ngasa baada ya bao la kwanza kwa mashabiki wa Simba sasa Habari kubwa ni kuwa Uongozi wa klabu hiyo unajipanga kumaliza soo kijanja "hebu fuatilia taarifa hii iliyowekwa kwenye ukurasa wa Wapenzi na Mashabiki wa Yanga."
Baada ya kufunga goli
alikimbia lilipo jukwaa la mashabiki wa Simba kisha akaonesha ishara kama
anavoonekana pichani.
Katika kipindi cha
michezo katika kituo fulani ndipo akaweka bayana kama nilivo andika katika post
fulani hapa, jinsi gani alivokataa dili la mamilioni kwenda El mereikh kisa
mapenzi yake kwa Yanga akaenda mbali zaidi jinsi gani klabu yake ilivomgeuka
kumsaidia kulipa deni la shilingi milioni 45 ambapo imemlazimu alipe mwenyewe
hivyo kupelekea mshahara wake wote ukatwe kwa ajili
ya ulipaji deni, hivyo aliwaomba msamaha mashabiki wa Simba na Azam kwa
kuwakosea kisa Yanga ambao mwishowe wamemgeuka.Akamalizia kusema anacheza
kwa jitihada kubwa kuisaidia timu yake ifanye vizuri ili amalizie miezi
michache iliyobaki katika mkataba wake.
Mashabiki, wapenzi
pamoja na viongozi wa Yanga hawakupendezwa na kauli ya Anko, kupitia Mkuu wa
kitengo cha habari Jerry Murro klabu yetu imeitisha mkutano na waandishi wa
habari ambapo atakuwepo Ngasa pamoja na msemaji wetu.
Hata kama ni kweli
klabu imemgeuka hakupaswa kuongea vile hadharani ikizingatiwa bado ni kijana
wetu, naomba busara zaidi itumike katika hili ikizingatiwa tuna mechi dhidi ya
Wa Botswana weekend hii, kasoro hii isitugawe, kama anavoonekana pichani
akiwaomba msamaha mashabiki wa Azam na Simba ndivo hivo hivo tuitumie picha hii
kama anatuomba msamaha mashabiki wa Yanga!
Tusubiri kesho nini
kitaendelea katika mkutano huo.
DAIMA MBELE NYUMA
MWIKO.
No comments:
Post a Comment