WANANCHI wa
kata ya Maweni Tanga wamepinga tangazo la ofisi ya Mkurugenzi wa jiji la Tanga
la kutamka viwanja walivyopima havitambuli kisheria na hivyo kuvirejesha na
kupimwa upya.
Wakizungumza
katika mkutano wa wananchi, wananchi hao, wamesema viwanja walivyopewa ni
halali na kupimwa kisheria kwa mujibu wa mamlaka ya Serikali ya kijiji na hivyo
kuitaka ofisi hiyo kutambua vyenginevyo wataacha kulipa kodi za viwanja vyao.
Viwanja
ambavyo vimetajwa kuwa vinahitaji kupimwa upya ni Maweni, Kichangani, Kasera na
Kange na wananchi kuja juu kwa madai baadhi yao wameanza kujenga na baadhi yao
kuhamia na familia zao.
Kwa upande
wake mkazi wa Kasera, Magreth Kashanga, na Salim Juma Ricco amesema migogoro ya
ardhi mingi inasababishwa na baadhi ya maofisa na hivyo kuitaka ofisi ya
mkurugenzi wa jiji kuacha kuibua mgogoro ambao haupo.
Zipo
taarifa kuwa baadhi ya wananchi waishio maeneo ya Kange wanapanga kuandaa
mkutano mkuwa wa siasa na Viongozi wa Chama cha mapinduzi CCM waila ya ya Yanga
ili kurudhisha kadi za chama hicho jambo ambalo litaleta mgogoro mkubwa kati ya
Halmashauri ya jiji na Chama Cha Mapinduzi CCM.
Viongozi wa
Serikali za mitaa hiyo minne waliwahi kugawa viwanja ambavyo baadhi yao
wamo wakazi wa Saru Magaoni ambao kwa jitihada za Mkuu wa Wilaya aliepita,
Halima Dendego alifanya suluhu ya kuwafidia viwanja baada ya kutakiwa kuondoka
maeneo yao kupisha ujenzi wa bandari mpya.
No comments:
Post a Comment