WATU saba wakiwamo
wanafunzi sita wa darasa la nne katika shule ya msingi Nyakasanda na Mwalimu wa
shule hiyo, Anderson Kibada wamekufa baada ya kupigwa na radi huku watu wengine
11 akiwemo Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Laurence Sesegwa (42) wakijeruhiwa.
Kaimu Mganga Mkuu
wa Wilaya ya Kasulu, Kigaga Daga alisema kuwa watu hao walifikwa na mauti hayo
kufuatia mvua kubwa zilizonyesha zikiambatana na radi zilizoanza majira ya saa
tano asubuhi zilizotokea katika kijiji cha Nyachenda wilaya ya Kasulu mkoani.
Mbali na Mwalimu
Kibada aliyekufa hapo hapo, Mganga huyo Mkuu wa Wilaya aliwataja wanafunzi kuwa
ni pamoja na Mary Steven (11), Severine Mussa (11) na Joseline Joseph (12).
Aliwataja wanafunzi
wengine waliofariki kuwa ni Joyness Simon (14), Nehemia Kepha (14) na Robin
Gabriel (14).
Alisema kuwa hadi
sasa wanafunzi wanne wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya
Kasulu ambao aliwataja kuwa Fadhila Emanuel (13), Matilda Moses (11), Bizimana
Manjo (12) huku wanafunzi wengine saba wakiruhusiwa baada ya hali zao kuwa
nzuri.
No comments:
Post a Comment