HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 21 February 2015

MKUU WA MKOA WA TANGA ASEMA TANGA SASA NI SHWARI, WAGENI MNAKARIBISHWA..!!



Na Godwin Henry.TANGA
MKUU wa mkoa wa Tanga Said Magalula  amesema hali ya kiusalama mkoani hapa  imeimarika na niyakuridhisha hivyo taasisi  na makampuni  yanakaribishwa kuandaa semina na mikutano pasipo kuwa na hofu yoyote ya kiusalama.
MKUU wa mkoa wa Tanga
Mh. Said Magalula
Magalula alisema hayo wakati akizungumza na maafisa rasilimali watu walio hudhuria semina ya mfuko wa mafao ya kustahafu GEPF iliyofanyika katika hoteli ya Tanga beach resort jijini hapa, ambapo ameutaka mfuko huo kuwa na utayari wakuandaa mkutano mkuu wa wanachama kwa mwaka 2015 mkoani hapa.
Baada ya tukio la mapigano ya kurushiana risasi baina ya majambazi na Polisi lililotokea kijiji cha Mleni kilometa tano kutoka katika vivutio vya Mapango ya Amboni biashara ya utalii na nyingine zimezorota mkoani hapa

Mhifadhi Msaidizi Mapango ya Amboni,Tabu Mtelekezo, amesema kwa sasa hakuna wageni wanaofika eneo hilo baada ya vyombo vya habari kupotosha eneo halisi lilipotokea mapigano baina ya majambazi na polisi.

Alisema toka tukio hilo lilipotokea hadi juzi wamepata wageni 16 ambapo ni idadi ndogo sana ikilinganishwa kabla ya tukio ambapo walikuwa wakipokea wageni 300 wa ndani na nje ya nchi.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa aliwaasa maafisa rasilimali watu mkoani hapa kutopokea rushwa kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuwashawishi watumishi wapya kujiunga na mifuko hiyo kwani nikinyume na sheria za nchi.
Nae Meneja wa masoko wa GEPF kutoka makao makuu Ayolce Ntukamazina amebainisha kuwa siri ya mafanikio ya mfuko huoni ubunifu wa huduma mpya na ubora katika utoaji wa mafao kwa wanachama wake.

Semina hiyo ya siku moja imehusisha maafisa rasilimali watu kutoka halimashauri za wilaya zote za mkoa wa Tanga pamoja na makampuni binafsi ukiwa ni mfululizo wa semina maalumu kwa nchi nzima huku Tanga ikiwa ni ya kwanza kupata fursa hiyo.

No comments:

Post a Comment