WAFANYABAISHARA
wa nyama wanotumia machinjio binafsi iliyoko Kata ya Pongwe, Tarafa ya Pongwe wameiomba
halmashauri ya jiji la Tanga kuwajengea machinjio ndogo itakayoweza kuwahudumia
Wafanya biashara wa nyama kutoka maeneo mbalimbali ya kata hiyo.
Wakizungumza
na mtandao huu wafanyabiashara hao wamesema Halmashauri ya jiji imewataka kuhama
kutoka machinjio wanayoitumia sasa ambayo waliijenga wao na kuhamia machinjio
ya Mbereselo ambapo watatozwa sh 5000/= kwa ng’ombe mmoja badala ya sh 2000/=
ambayo wanatozwa na Halmashauri ya jiji kama ushuru wa machinjio kwa sasa.
Mmoja wa
wafanya biashara hao aliyejitambulisha kwa jina la Focus Augustino amesema
wanaiomba halmashauri ya jiji kupitia Diwani wa kata ya Pongwe Bi.Uzia Komba
kuwajengea machinjio ndogo kama iliyojengwa amboni kwani haitakuwa rahisi kwa
wao kuitumia machinjio ya Sahare ambayo iko mbali na mji wa Pongwe.
Mji wa
Pongwe ni miongoni mwa miji inayokuwa kwa kasi hivi sasa ambapo Bishara
mbalimbali zimeshamiri hasa ya nyama kutokana na fursa za viwanda zinazo
uzunguka mji huo.
No comments:
Post a Comment