TIMU ya Coastal
Union ya Tanga imesema kuwa itahakikisha inapambana vilivyo ili kuweza
kuhakikisha inachukua pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City kwenye mechi ya
Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayochezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani.
Coastal Union
itangia kwenye mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao ya mzunguko
wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City
iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilipatikana kwa njia ya penati.
Akizungumza
maandalizi ya kuelekea mchezo huo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga
alisema kuwa maandalizi ya kuelekea mechi hiyo imekamilika kwa asilimia kubwa
kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni.
Amesema kuwa
mipango yake mikubwa ni kuhakikisha wanafuta machungu ya kufungwa na Yanga bao
1-0, kwenye mechi yao ya Ligi kuu iliyochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani
jambo ambalo halikuwafurahisha mashabiki na wapenzi wa soka.
Aidha amesema
kutokana na kikosi chake kuendelea kuimarika kila mchezo wanaokuwa wakicheza
wana matumaini makubwa ya kupata ushindi ambao utawawezesha kusogea kwenye
nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo.
Alisema
kuwa ligi kuu msimu huu imekuwa ni ngumu sana lakini kubwa ni kujipanga hivyo
wamejipanga vizuri kwa umakini mkubwa lengo likiwa kukiwezesha kikosi hicho
kinapata matokeo mazuri
No comments:
Post a Comment