KLABU ya Manchester
United inaongoza mbio za kumuwania beki chipukizi wa klabu ya Feyenoord Terence
Kongolo katika majira ya kiangazi. Kongolo yuko katika rada za kocha wa zamani
wa Feyenoord Ronald Koeman kwenda Southampton wakati Manchester City nao
wameonyesha nia ya kumuunganisha nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 na kaka
yake Rodney ambaye anacheza katika kikosi chao cha vijana chini ya umri wa
miaka 18.
Hata hivyo, United
ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili Kongolo huku Louis van Gaal akitajwa
kumhusudu beki huyo wa kati kwa kumpa nafasi ya kuitumikia timu ya taifa ya
Uholanzi kwa mara ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana. Van
Gaal atakuwa sokoni kutafuta mabeki katika majira ya kiangazi na atakuwa
akiangalia kusajili mabeki wenye ubora kama Mats Hummels au Diego Godin.
Inawezekana Klabu ya
Manchester City Huenda ikamuachia kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo na timu ya
taifa ya Ivory Coast Yaya Toure, kama watafanikisha kumsajili kiungo wa klabu
ya Juventus Turin na timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba katika usajili wa
majira ya Joto.Katika siku za hivi karibuni Yaya Toure ameonyesha kiwango cha
chini akiwa na klabu yake, baada ya kutokuimarisha safu ya kiungo ya Manchester
City inayoongozwa na mchezaji wa timu ya Taifa ya Uhispania David Silva.
No comments:
Post a Comment