VINARA
wa Ligi Kuu England, Chelsea, hatimaye wamekamilisha Usajili wa Mchezaji wa
Kimataifa wa Colombia, Juan Cuadrado, kutoka Fiorentina baada ya kukwama
kutokana na Dili za Uhamisho za Wachezaji wao Andre Schurrle na Mohamed Salah
kunasa.
Lakini
baada ya mambo kwenda sawa kwa Uhamisho wa Kudumu wa Andre Schurrle kwenda
Wolfsburg kwa Pauni Milioni 22 na Mohamed Salah kutua Fiorentina kwa Mkopo wa
Miezi 6, Chelsea imeweza kumnunua Juan Cuadrado kwa Dau linalodaiwa kufikia
Pauni Milioni 26.8.
Inaaminika
Cuadrado, ambae alishapimwa Afya yake mapema Leo huko Stamford Bridge, atasaini
Mkataba wa Miaka 4 na Nusu.
Yakubu
arejea England
Nae
Mchezaji wa Kimataifa wa Nigeria, Yakubu Aiyegbeni, amerejea England baada
kusaini kuichezea Reading kama Mchezaji Huru na hiyo itakuwa Klabu yake ya 6
kuichezea Nchini humo.
Akiwa
England, Yakubu, mwenye Miaka 32 na ambae Klabu yake ya mwisho ni Al Rayyan ya
Qatar, ashawahi kuzichezea Klabu za Portsmouth, Middlesbrough, Everton,
Leicester City na Blackburn Rovers.
Yakubu
aliihama Blackburn Rovers Mei 2012 na kwenda huko China kuichezea Guangzhou FC.
Zaha
arudi Palace
Crystal
Palace wamemsaini tena Winga wao Wilfried Zaha kwa dili ya kudumu kutoka
Manchester United.
Zaha,
mwenye Miaka 22, alihamia Man United Miaka Miwili iliyopita kwa Dili ya Pauni
Milioni 15 lakini alishindwa kupata Namba na Msimu huu akawa huko Palace kwa
Mkopo.
No comments:
Post a Comment