Sanjari
na hilo amehimiza ujenzi wa maabara akisema kuwa ingawaje mambo yameendelea
kwenda vizuri lakini bado kuna haja ya kujidhatiti katika upatikanaji wa samani
mbalimbali kama vile meza,viti,milango,madirisha na vitu vingine
vinavyohitajika katika hatua ya umaliziaji kazi hiyo.
Kalinjuna
ameyasema hayo kwenye kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika hivi karibuni
wilayani humo.
Kwa
upande wake katibu tawala wa wilaya ya Korogwe Lameck Stanley aliyehudhuria
kikao hicho aliwataka wajumbe kuongeza jitihada za kuboresha huduma za afya
kwenye hamashauri hiyo ya mji ili ambao unaonekana kkukua kwa kasi ili ziweze
kuendana na hali halisi ilivyo.
Amesema
kwa sasa mji wa Korogwe unaendelea kukua kwa kasi na inawezekana muda siyo
mrefu wilaya ikapata hadhi ya kuwa mkoa huku akieleza kuwa itashangaza hadhi ya
namna hiyo inapatikana huku huduma za msingi kama vile afya bado zikiwa hazijaimarika
kulingana na wakati uliopo hivi sasa.
Naye Mwenyekiti
wa CCM Korogwe mjini Immanuel Charles ameelezea umuhimu wa suala la
mgawanyo wa mali kati halmashauri ya mji Korogwe na ile ya wilaya akisema
kwamba hatua hiyo inapaswa kuwekwa vizuri njia ambayo italeta tija kwa vizazi
vijavyo.
Ushauri
huo wa Charles aliutoa kutokana na kikao hicho kuibua hoja kwamba bado kuna
baadhi ya mambo hayajawa sawa tangu kugawanywa kwa halmashauri hizo ambapo
awali ilikuwepo moja tu ile ya wilaya ambayo imeizaa Mji Korogwe huku baadhi ya
wajumbe wakiomba kukutanishwa kupata muafaka.
No comments:
Post a Comment