WAKATI nchi ikijiandaa kwa Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, asasi za kiraia na kijamii nchini zinazotaka kutoa huduma ya elimu ya uraia na ya mpiga kura kuhusu Katiba Inayopendekezwa, zimetakiwa kuomba vibali vya kufanya hivyo, vinginevyo hazitaruhusiwa kutoa elimu yoyote juu ya katiba hiyo.
Jaji Damin Lubuva(Mwenyekiti wa NEC)
|
Agizo
hilo lilitolewa jana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na ile ya Zanzibar
(ZEC). Tume hizo zilisisitiza kuwa asasi zinapaswa kufanya hivyo kabla ya
Februari 10 mwaka huu, yaani Jumanne ijayo.
Katika
taarifa yake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Mallaba alieleza kuwa kwa
kuzingatia Sheria ya Kura ya Maoni ya mwaka 2013 Kifungu cha 5 na 6(1)(b), NEC
na ZEC ndizo zilizopewa mamlaka ya kusimamia na kutoa kibali kwa Asasi za
Kiraia na Kijamii ambazo zina nia ya kutoa Elimu ya Uraia na ya Mpiga Kura
kuhusu Katiba Inayopendekezwa.
Aliongeza
kuwa chini ya kifungu hicho cha sheria, Asasi ambayo haitapata kibali kutoka
NEC na ZEC, haitaruhusiwa kutoa Elimu ya Uraia au Elimu ya Mpiga Kura kuhusu
Katiba Inayopendekezwa.
“Pia
Tume zinapenda kuzialika Asasi za Kiraia na Kijamii zenye nia ya kutoa Elimu ya
Uraia au ya Mpiga Kura kuhusu Katiba Inayopendekezwa kuwasilisha maombi yao
Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Posta House) na Makao Makuu ya Tume
ya Uchaguzi ya Zanzibar,
Jaji Warioba |
“Vigezo
vingine ni pamoja na kuwa tayari kujigharimia katika kutoa Elimu ya Uraia na
Elimu ya Mpiga Kura, Isiwe na taarifa za kuvuruga amani au kuchochea fujo,
watendaji wake wawe na uwezo wa kutosha wa kutoa Elimu ya Uraia na ya Mpiga
Kura utakaoiwezesha Asasi hiyo kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.
Iwasilishe
maeneo au majimbo inayotaka kutoa elimu hiyo, itoe na kukabidhi nakala za
machapisho yatakayotumika na mwisho iwasilishe ratiba itakayoendesha elimu
hiyo.
“Katika
kutuma maombi hayo, asasi zote zinatakiwa kuambatanisha maombi yao na cheti cha
usajili, katiba ya asasi, majina ya viongozi wa juu wa asasi, anuani kamili ya
makazi na namba za simu za ofisini na za viongozi.
Viambatanisho
vingine ni zana za Elimu ya Uraia na Elimu ya Mpiga Kura (vijarida,
vipeperushi, mabango, vipindi vilivyorekodiwa, fulana na kadhalika).
“Na
mwisho kila asasi iambatanishe na ratiba itakayoonesha tarehe, mahali na muda
watakaotoa Elimu ya Uraia na ya Mpiga Kura.” Kwa mujibu wa sheria, Elimu ya
Uraia na ya Mpiga Kura kwa ajili ya Katiba Inayopendekezwa, inapaswa kufanyika
siku 60 kabla ya Kura ya Maoni.
Akihutubia
wakati wa maadhimisho ya Miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM, Rais Jakaya Kikwete
alisema maandalizi ya Kura ya Maoni itakayopigwa Aprili 30 mwaka huu,
yanaendelea vizuri.
CHANZO:HABARI LEO
No comments:
Post a Comment