Jeshi la polisi mkoani Tanga limefanikiwa kuwatianguvuni watu
wawili kwatuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya
mirungi bunda 40 sawa na kilo 8 ,walipokuwa wakizisafirisha kutoka Lushoto
kuelekea Dar es Salaam wakitumia Basi kampuni ya Shambalai lenye namba za
usajili T628.
Tukio hilo limetokea hapo jana majira ya saa 4 na robo asubuhi katika
kijiji cha kwasanda kata ya Makuyuni Tarafa ya Mombo Wilaya ya Korogwe ,mara
baada uya askari polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema.
Akithibitisha kutokea kwatukio hilo Kaimu kamanda Mkoani hapa Juma
Ndaki amesema watuhumiwa ,walio shikiliwa ni Michael Charles mwenye umri wa
miaka26,na Amir Islam miaka23 wote wakiwa ni utingo.
Ndaki ameongezea kuwa mara baada ya kubanwa watuhumiwa hao walikiri
kufanya biashara hiyo kwa lengo
lakujipatia kipato. na punde watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi wa
awali kukamilika.
No comments:
Post a Comment