MKAZI wa
kijiji cha Nyakabanga kata ya Butelankuzi, Bukoba vijijini, Eliud Charles (30)
anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia gauni la mkewe, Velidiana Eliud
kutokana na wivu wa mapenzi.
Inadaiwa
kabla ya kujinyonga jana saa 12 asubuhi, alimkata mapanga mkewe akimtuhumu
kutembea nje ya ndoa. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe
alisema wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa muda mrefu.
Inadaiwa
baada ya kujibizana kwa maneno, mume alimkata mkewe sehemu za mdomo na mkono
wake wa kulia. Kamanda Mwaibambe alisema mume aliingia ndani ya nyumba yake na
kuchukua gauni la mkewe na kujining’iniza darini katika sebuleni ya nyumba
yake.
Mwaibambe
alisema Velidiana amelazwa katika Hospitali ya Ndolage wilayani Muleba na hali
yake inaendelea vizuri. Mwili wa marehemu ulichukuliwa na ndugu zake na kuzikwa
baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment