Watusaba wanao sadikiwa kuwa nimajambazi wamevamia gari aina ya Scania yenye namba T 111 BDY iliyo
kuwa na watu watatu na kuwajeruhi kisha kuwapora fedha taslimu sh
1,577,000 pamoja na simu za mkononi nakutokemea kusiko
julikana.
Tukio hilo limetokea mnamo aprili9 katika kijiji cha michungwani kata
ya segera tarafa ya mkumburu ambapo gari hilo lilikuwa likitokea dar es
salaam kuja Tanga, nandipo majambazi hayo yaliweka magogo njiani kwalengo lakulizuia gari hilo nakisha kutokea
na silaha za jadi wakiwashambulia watu walio kuwa ndani ya gari hilo.
Kaimu kamanda juma ndaki amesema katika gari lililo vamiwa
alikuwemo Yahaya Salimu mwenyemiaka 32 mwarabu na mfanya biashara
mkazi wa sinza dar es salam ambaye alishambuliwa pamoja na wenzake.
Sanjari na hayo jeshi la polisi mkoani hapa lina endesha msako mkali
kuwatafuta watu hao walio husika katika unyang’anyi huo ilikuweza kuwafikisha
kwenye vyombo vya dola.
No comments:
Post a Comment