Na Masanja Mabula .Pemba
Imeleezwa
kuwa asasi ya kiraia zina nafasi kubwa katika kufanikisha udhibiti wa
uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya Tabianchi .
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete Pemba Hassan Khatib Hassan wakati
akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Jimbo la Mtabwe
Amesema
kuwa katika kufanikisha hilo asasi za kiraia zinatakiwa kuwa mstari wambele
kuwaelimisha wananchi athari za mabadiliko ya Tabianchi yanayotokea siku hadi
siku.Mkuu huyo wa Wilaya ameitaka Jumuiya hiyo kuhakikisha kwamba maeneo ya
wazi ambayo yameathirika kwa kukatwa miti ovyo yanarejeshwa katika hadhi yake
kwa kupandwa miti
Naye Diwani wa Wadi ya Mtambwe Bw Hamad Mjaka Bakar amesema kuwa lengo Jumiya hiyo ni kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira pamoja kutatua kero zao .
No comments:
Post a Comment