HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 7 January 2015

WANNE WAUAWA KIKATILI PONGWE KWA WIZI WA NG'OMBE.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga "Frasser kasai akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni mwandishi wa mtandao huu Rebeca Duwe.

NA REBECA DUWE.TangaWatu wanne wameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa  kutumia Silaha mbalimbali za jadi hadi kusababisha vifo vyao kwa kosa la kuiba Ng'ombe mmoja mwenye thamani ya shilingi laki saba na kisha kukamatwa wakiwa na ng'ombe huyo.
Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Tanga Frasser Kashai amesema tukio hilo limetokea manmo january 5 mwaka huu majira ya saa 20:00 usiku katika  kijiji cha Maranzara Tarafa ya Pongwe Wilayani Tanga.

Kamanda Kashai  amewataja watuhumiwa hao waliouawa kuwa ni Mwenshehe Abasi(29) mkazi wa Pongwe,Edwin Kamugisha (25) mkazi wa  Pongwe , Bakari,Jamse Erick (22)mkazi wa Kange na Juma Bakari ambaye hajatambulika umri wala makazi .

Aidha amesema inadaiwa kuwa baada ya ng'ombe huyo kuibiwa wananchi walifuatilia nyao za ng'ombe na ndipo walipo wakuta  watuhumiwa hao wanne wakimfunga ng'mbe huyo kwenye mti hivyo wananchi hao wakaanza kuwashambulia na kuwasababishia vifo vyao.


Amesema baada ya wananchi hao kufanya kitendo hicho cha mauaji waliacha miili ya marehemu hao polini na kisha kutoweka ktika eneo hilo na polisi baada ya kupata taarifa za tukio hilo kwa raia wema walienda eneo hilo na kukuta tayari watuhumiwa hao wameshauwawa.

Amesema kufuatia mauaji hayo Jeshi  la Polisi limefanya Msako mkali na kufanikiwa kuwakamata  watuhumiwa watano waliohusika na mauaji hayo ya kujichukulia sheria mkononi ambao walifahamika kwa majina yao Abdi Mohamedi (29)  Kombo Mrami (23) Maendo Juma (20), Hakimu Omari (53) na Issa Bakari (53) na watuhumiwa wote watano ni wadigo wakazi wa Maranzara.

Hata hivyo amesema kuwa marehemu watatu walikabidhiwa kwa ndugu zao kwa ajili ya mazishi baada ya uchunguzi wa daktar na marehehemu mmoja bado amehifadhiwa katka hospital ya Mkoa Bombo kutokana na kutojitokeza kwa ndugu zake .

Mbali na hayo watuhumiwa wote wa mauaji hayo watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa awli kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake.

Na katika tuko jingine Kamanda Kashai alisema mnamo january 6 mwaka huu majira ya saa tisa usiku katika kjijij cha Hangara wilayani Kilindi Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mohamedi Salim (32) alivunjiwa mlango wa nyumba yake na mtu/watu wasiofahamika na kisha kuiba Pikpik yenye namba za usajli T.973 CSU,CHESIS NO.LJBPJ82 BXDIC2182 yenye namba nyekundu aina ya Kinglion yenye thamani ya shilingi milion moja laki na nne.

Alisema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hlio na msako mkali unaendelea ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.

Sambamba na hilo jeshi la polisi limewataka wanchi kutojichukulia sheria mkononi kwa kuwajeruhi au kuwauwa watuhumiwa wa makosa mbalimbali ya jinai na badala yake wawafikishe katika vyombo vya sheria na siyo kujichukulia uamuzi wa kuwaopiga na kuwauwa kwani kazi ya kuhukumu ni jukumu la mahakama kwa mujibu wa sheria ya nchi.

No comments:

Post a Comment