Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara
inaingia raundi ya tatu kwa nusu ya pili ambapo wawakilishi wa Tanga kwenye
michuano hiyo Wana kimanumanu African
Sport wameendelea kupamabana ili kukata tiketi ya kucheza ligi kuu Tanzania
Bara msimu ujao wa 2015/16. Katika Mchezo wa kwanza African Sport waliichapa
African Lyon 1-0 na baadae kukubali kipigo cha 1-0 dhidi ya Lipuli Fc ya mkoani Iringa Mchezo uliopigwa
katika Dimba la kumbukumbu ya Samora mkoani Iringa. A.Sprt walizindika tena kwa
ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Dar Es Salaam.
Wana kimanumanu African Sport |
Baada ya kuishinda African Sport Lipuli fc imepanda kwa mpaka nafasi ya
pili kwenye msimamo wa kundi hilo ikiwa na Points
26. Kabla ya kuwakabili African Sport Lipuli waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi
ya wababe wa DSM Friends Rangers. Mchezo
unaofuata Lipuli watakuwa wenyeji wa
African Lyon katika uwanja
kumbukumbu ya Samora mkoani Iringa.Huo ni mchezo wa kiporo kwa Lipuli ambayo
iko nyuma kwa mchezo mmoja tofauti na timu nyingine.
Kikosi cha Lipuli Fc |
Nayo Kurugenzi FC ilianza vibaya mzunguko wa pili
kwa kupoteza dhidi ya Tesema FC mchezo uliochezwa katika Dimba la mkwawani hapa
jijini Tanga na baadae ikazinduka na kuichaba 2-0 timu ya Polisi Dar Es Salaam,
kwa matokeo hayo Kurugenzi inakamata nafasi ya 9 ikiwa imejikusanyia Point 16
na Mchezo unaofuata itawakabili
wauza mitumba wa Ilala “Ashanti fc”
katika Uwanja wa Karume jiji DSM.
MSIMAMO WA
KUNDI A;KWA TIMU ZA JUU”
Majimaji -28
Lipuli -26
African Sport -26
Friends -24
RATIBA YA MECHI
ZIJAZO KWA AFRICAN SPORT
Jan 12- African Sport Vs Ashanti(Mkwakwani)
Jan 15-African Sport Vs Tesema (Mkwakwani)
Jan 18-African Sport Vs Villa Squad (Mkwakwani)
RATIBA YA MECHI
ZIJAZO KWA LIPULI FC
Jan 7- Lipuli Vs African Lyon (Kumbukumbu ya Samora Iringa)
Jan 11- Lipuli Vs Majimaji (Songea)
Jan 14 Lipuli Vs Mlale JKT (Songea)
No comments:
Post a Comment