HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 28 December 2014

KIJANA MKAZI WA PONGWE APOTEZA MAISHA PIKNIK PANGANI BEACH.


Fukwe za Pangani.

Mkazi wa Pongwe jijini Tanga, Hamis Adam (17) anahofiwa kufa maji baada ya kuzama katika Bahari ya Hindi wakati akiogelea na wenzake na mwili wake haujapatikana.

Hamis alikuwa na vijana wenzake ambao walikwenda kwenye ufukwe wa Muhembo uliopo Wilaya ya Pangani kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa kuogelea.

Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Fresser Kashai zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Dec 25 saa 10.00 jioni katika ufukwe wa Mhembo ambao ni maarufu kwa vijana kwenda kuogelea.

Katika tukio hilo vijana wengine wawili waliweza kuokolewa na waokoaji kabla ya kuzama kwenye maji marefu na Hamis akiwa hajulikani alizamia upande gani.

“Licha ya jitihada kubwa kufanyika za kumwokoa kijana huyu lakini ilishindikana, inawezekana alivutwa na mawimbi ya maji yaliyokuwa na nguvu kubwa,” alisema Jumaa Faki, mmoja wa waokoaji waliowaokoa vijana wawili ambao walirejea nyumbani baada ya kupewa huduma ya kwanza.

Vijana wengi wa Pongwe wamekuwa na mazowea ya kwenda Piknik hasa wakati wa sikukuu za Krismas huku wengi wao wakia si wazoefu wa kuogelea hali inayohatarisha usalama wao, Mwishoni mwa Mwaka jana Vijana wawili wa Muheza walipoteza maisha katika safari kama hiyo kwenye fukwe za Pangani.

Katika tukio lingine, mkazi wa Usagara jijini Tanga, Hussein Mohamed (35) amekufa baada ya kushambuliwa na wananchi waliomtuhumu kuvunja nyumba na kuingia ndani kwa nia ya kuiba.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kashai alisema jana kuwa Hussein alikufa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo alikopelekwa kupatiwa matibabu baada ya kuokolewa wakati akipewa kipigo.

No comments:

Post a Comment