ALIYEKUWA
mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Serikali ya kitongoji cha Idodomiya kijiji cha
Kanoga na mfanyakazi wake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, wameuawa kwa kupigwa kwa mapanga.Katibu wa
chama hicho Wilaya, Rajabu Hamisi alisema kuwa mauaji hayo yalitokea juzi
nyumbani kwake katika kijiji cha Kanoga wilayani Kaliua mkoani humo.
Alimtaja
aliyekuwa mgombea wao aliyeuawa kuwa ni Wilsoni Masanilo (35) mfanyabiashara wa
ng’ombe na mfanyakazi wake ni Juma Ujege (30).Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,
Suzana Kaganda alikiri kuwapo kwa mauaji hayo na kusema taarifa za awali
zinaonesha kwamba wameuawa na majambazi walikuwa wanatafuta fedha walizokuwa
wameuza ng’ombe.
No comments:
Post a Comment