Na
Masanja Mabula.Pemba Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa tuhuma za wizi wa mafuta ya Diesel Mali ya Kampuni ya H/YOUNG inayojenga barabara ya Makangeni -Kinazini shehia ya Mtambwe Kusini .
Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa , Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Wete Omar Athman Mussa amesema kuwa kati wa watu hao wawili ni wafanyakazi wa ulinzi wa Kaampuni hiyo .
Amesema kuwa mtuhumiwa wa kwanza ni Yussuf Kaim Makame (30) ambaye amekamatwa akiwa na lita 43 za mafuta na alikamatwa na wananchi wanaunga mkono falsafa ya Polisi Jamii .Amewataja walinzi wa kampuni hiyo wanaohusishwa na wizi huo ni Bakar Ali Bakar (27) pamoja na Makame Khamis Omar (25).
Amesema kuwa watu hao wamekamatwa jana majira ya saa moja usiku na kwa sasa wanaendelea kuhojiwa na watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika.
No comments:
Post a Comment