African Sport “Wana Kimanu Manu” |
Wawakilishi
wa Tanga katika michuano ya Ligi Daraja la Kwanza African Sport “Wana Kimanu Manu” wameendelea kujiweka
katika nafasi nzuri ya kupanda Daraja na kuingia Ligi Kuu ya Soka
Tanzania Bara 2015/16 baada ya hapo jana kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao
2-1 dhidi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni(K.M.C) maarufu kama Tesema
Fc.
Mchezo
huo ulichezwa katika Dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga kuanzia saa 10 jioni
ambapo African Sport walikuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 34 kwa njia ya
penalt iliyotolewa na mwamuzi baada ya Mshambuliaji wao tegemeo Ahmed
Shiboli kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari la Tesema Fc, na penalt hiyo
kupigwa na Ali Ramadhani a.k.a “KAGAWA”.Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika
African Sport walikuwa mbele kwa bao kwa 0.
Winga
machachari wa A.Sport Maulid Abas aliyeingia kipindi cha pili alikuwa moto kwa
safu ya ulinzi ya Tesema na kunako dakika ya 64 ya mchezo aliambaa na mpira
winga ya kushoto huku akuwahadaa mabeki wa Tesema kwa chenga za maudhi kisha
akaingiza krosi ya chinichini iliyomkuta mshabuliaji Ahmed Shiboli naye
hakufanya ajizi akaburuza pasi ya chinichini ambayo ilimshinda mlinda mlango
wa Tesema na kumfikia Nahodha wa African Sport James Mend ambaye alikuwa
pekeyake na kupasia nyavu kiulaini.
Tesema
Fc walipata bao la kufutia machozi muda mfupa kabla ya mchezo kumalizika dakika ya 84 baada
ya kutokea piga nikupige langoni kwa African Sport na Ben Ngasa kuipatia timu yake
bao.Kwa ujumla African Sport walitawala kipindi cha kwanza cha mchezo na Tesema kipindi
cha pili hasa mwishoni ambapo mashabiki wa African Sport walikuwa nyumbani walijikuta
wakiomba mpira uishe.
Nyota
wa mchezo huo alikuwa winga nambari 7 wa Tesema FC Seif Abdallahaman Karihe.
Kwa
matokeo hayo A.Sport wamefikisha Points 32 katika nafasi ya pili baada ya
michezo 16 na mchezo uja watakuwa nyumbani kuwakaribisha Villa Squad hapo
January 18.
Msimamo kwa timu 6 za juu(kwa Mujibu wa Tovuti ya TFF)
Pos
|
Team
|
Pld
|
W
|
T
|
L
|
Goals
|
Diff
|
Pts
|
1
|
Majimaji
|
16
|
10
|
5
|
1
|
21:8
|
13
|
35
|
2
|
African
Sports
|
16
|
10
|
2
|
4
|
20:14
|
6
|
32
|
3
|
Lipuli
|
16
|
7
|
7
|
2
|
11:7
|
4
|
28
|
4
|
Friends
Rangers
|
16
|
6
|
8
|
2
|
17:12
|
5
|
26
|
5
|
Tessema
|
16
|
6
|
3
|
7
|
9:12
|
-3
|
21
|
6
|
Ashanti
United
|
16
|
5
|
4
|
7
|
18:23
|
-5
|
19
|
No comments:
Post a Comment