NA
REBECA DUWE,TANGA.
Jeshi la polisi mkoani Tanga
linawashikilia watu watatu akiwemo mwanamke mmoja kwa tuhuma za
kupatikana na madawa ya kulevya aina ya Mirungi yanayokadiriwa kuwa takribani
kilogramu 440 ambayo walikuwa wakiyasafirisha kwa kutumia basi la abiria kutoka
Arusha kuelekea jijini Dar es salaam.
Madawa hayo ya kulevya aina ya
mirungi ambayo yamekamatwa inadaiwa kuwa yalikuwa yamehifadhiwa kwenye mifuko
ya viroba ipatayo 18 ambavyo vilkikuwa vimehifadhiwa kwenye basi hilo
vikisafirishwa kwa ajili ya kuelekea Jijini Dar es salaam ambako watuhumiwa hao
wanadaiwa kuendesha shughuli zao hizo.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Tanga
Juma Ndaki alitoa taarifa hiyo Jan alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake alisema watuhumiwa hao walikamatwa huko
eneo la Chekelei wilayani Korogwe ambapo watuhumiwa bado wako mikononi mwa
polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Ndaki aliwataja watuhumiwa hao kuwa
Sara Mbwambo (38) mfanyabiashara,Rodison Sam (24) kondakta na Godfrey Machumbe
(30) tani boi wote ni wakazi wa jiji la Dar es salaam na wanaelezwa kuwa
walisafirisha mirungi hiyo kwa kutumia gari lenye nambari T 244 DXQ mali
ya kampuni ya Dar express.
Kwa mujibu wa kamanda Ndaki ni
kwamba watuhumiwa wote hao baada ya mahojiano ya awali na polisi wamekiri
kuhusika na biashara hiyo ya usafirishaji wa madawa hayo ya kulevya aina ya
Mirungi ambapo watafikishwa mahakamani mara baada ya upepepezi wa awali
unaofanywa na jeshi la polisi kukamilika.
“Watu watatu wanashikiliwa na polisi
wakituhumiwa kupatikana na Miringi viroba 18,walikuwa wakisafirisha kwa basi
toka Arisha kwenda Jijini Dar es salaam ambapo katika mahojiano ya awali wote
wamekiri kuhusika na biashara hiyo na uchunguzi ukikamilika tutawafikisha
mahakamani”alisema Ndaki.
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa
lindi la wananchi kujihusisha na biashara hiyo haramu kaimu kamanda huyo wa
polisi mkoa wa Tanga ametoa rai kwa umma wa watanzania kuepuka kujihusisha na
uendeshaji wa shughuli hizo ambazo siyo halali ambazo pia huleta madhara
makubwa kwa Taifa.
Alisema siyo vyema kwa wananchi
kuendesha biashara hizo ambazo tayari zilishapigwa marufuku kisheria ambapo
aliwataka kubadilika kwa kufanya kazi halali zitakazowasaidia kuendesha maisha
yao badala ya zile zenye fedha nyingi ambazo zinaweza kuwapotezea ndoto zao
walizokuwa nazo maishani.
Mbali na kukamatwa kwa
watuhumiwa hao wa Mirungi kamanda Ndaki pia alisema madawa ya kulevya aina ya
bangi kilogramu 64 yamekamatwa yakiwa yamechanganywa na magunia ya vitunguu
yakisafirishwa kwa kutumia gari aina yaToyota Coaster lenye nambari za
usajili T 560 ASJ.
Kamanda Ndaki alisema katika tukio
hilo lililotokea Mombo Motel hakuna mtu aliyekamatwa akihusishwa na mzigo huo
wa bangi kutokana na anayedhaniwa kuhusika kufanikiwa kukimbia wakati wa
uchunguzi uliolenga kumtambua na polisi wanaendelea kumsaka ili hatua za
kisheria kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment