Wachuuzi wa Samaki wakiwa Sokoni hapo kusubiri wavuvi |
Na Godwin Henry
.Tanga
Soko maarufu la
Samaki la Deep Sea la jijini Tanga liko katika hali yatari kutokana na uchafu
uliokithiri kusambaa kwenye soko hilo.Wakiongea na mwandishi wa Habari hizi
baadhi ya wafanyabiashara wa Soko hilo wamebainisha kuwa hakuna dampo la kutupa
takataka hali ambayo inawalazimu watuamiaji kutupa hovyo.
Mwandishi
ameshuhudia takataka nyingi zikiwa zimejikusanya kando ya bahari na pembezoni
migahawa ya chakula na kutoa harufu mbaya.
Huduma Ya Vyoo
Huduma ya vyoo nayo
imesitishwa kwa muda mrefu sasa na kuwalazimu watumiaji wa soko hilo hasa Mama
Ntilie na Wavuvi kujisaidia kwenye vichaka kando ya Bahari hali inayohatarisha
afya zao kwani ni rahisi kutokea kwa magonjwa ya milipuko.
Baadhi ya wavuvi
wamezungumza na mwandishi wa habari hizi na kueleza kuwa vyoo ambavyo
vilijengwa kwenye Soko hilo vimeharibika kutokana kujengwa chini ya viwango.
“Ni muda mrefu sasa
tunajisaidia kwenye vichaka kando ya bahari kwa sababu hatuna njia nyingine”
alisema Mkombozi Athumani ambaye ni mvuvi.
Huduma za Maji,Umeme na Barabara
Nazo huduma muhimu
za Umeme na maji zimesitishwa pia kutokana na usumamizi mmbovu na kusababisha
adha kubwa kwa watumiaji wa soko hilo kwani Samaki huitaji kuandaliwa kwa usafi
na maji ya kutosha kabla ya kuuzwa kwa mteja.
Barabara inayoingia
Sokoni hapo ni mbovu na ina mashimo makubwa kiasi ambacho mabari yanashindwa
kuingia na kulazimika kupaki kando ya barabara ya kwenda bandarini eneo amblo
si salama kwani malori makubwa ya mizigo hupita kwa kasi.
Makusanyo ya Ushuru.
Pamoja na Matatizo
hayo Halmashauri ya jiji la Tanga
kupitia watendaji wake imeendela kuwatoza kodi watumiji wa soko hilo wa sh
3000/= kwa wavuvi kulingana na samaki aliowavua,sh 200/= kwa kila ndoo 1 ya
Samaki kwa Wafanyabiashara na leseni ya sh 16000/= kwa mwaka kwa Mama Ntilie
wanaopika na kuuza vyakula soko ni hapo.
Soko hilo kongwe
linatumiwa na zaidi ya Wafanyabiashara 50 wanaouza samaki, wavuvi kutoka
maeneno mbalimbali, Migahawa zaidi ya 12 ya Mama Ntilie na wanunuzi wengi
kutoka ndani na nje ya jiji la Tanga.
Uongozi wa Jiji
Mwandishi wa Habari
hizi alishindwa kuupata Uongozi wa Halmashauri ya jiji la Tanga ili kutoa
majibu ya kero hizo kutokana na Ofisi zake kufungwa kupisha sikukuu ya miaka 51
ya Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment