MOTO
mkubwa umezuka na kusababisha
taharuki katika uwanja wa ndege wa Majanimapana Tanga, jana majira ya saa tisa alasiri
na kuwalazimu abiria kusubiria zaidi ya saa tatu kuendelea na ratiba zao.
Moto huo uliochukua zaidi ya saa 13
kuzimwa kwa kusaidiana na wanafunzi wa Chuo cha Anga cha Kijeshi umeripotiwa
kuanzia kwenye nyasi sehemu ya kurukia ndege.
Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Tanga, Juma Ndaki, aliwaambia waandishi wa habari leo kuwa tukio hilo ambalo
chanzo bado hakijafahamika liliathiri ratiba ya safari kwa wasafiri wa kisiwani
Pemba na Unguja.
Vikosi vya zimamoto Tanga |
Mmoja
ya wasafirishaji wa kampuni ya ndege ya Coastal Aviation Mohamed Ahmad, amesema
ndege yao ililazimika kuzunguka karibu dakika 15 angani kutafuta mwelekeo wa
kutua kukwepa moshi uliokuwepo jirani na njia ya kurukia ndege na kisha kutua
salama majira ya saa 10:00 jioni.
Nao wananchi wanaoishi pembezoni mwa
uwanja huo ambao ni wa pekee Mkoani Tanga wameeleza kuwa sio
jambo la kushangaza kushuhudia moto kwenye uwanja huo jambo lililoungwa mkono
na Afisa wa uwanjani hapo ambae hakutaka jina lake kutajwa.
No comments:
Post a Comment