Kamanda wa usalama barabarani Mkoa wa Tanga, Abdi Issango(kushoto) akizungmza na bodaboda Tanga |
WAFANYABIASHARA wa pikipiki maarufu kama (Bodaboda),
wameitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na halmashauri ya
jiji la Tanga kuwapunguzia wingi wa kodi vyenginevyo biashara hiyo inaweza kuwa
ngumu kwao.
Wakizungumza katika kikao kilichowakutanisha, jeshi la
polisi, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na halmashauri ya jiji la Tanga,
wafanyabiashara hao wamesema kukuwa kwa sekta hiyo isiwe kafara kwa kuongezewa
kodi.
Wamezitaja kodi hizo ni shilingi 25,000 wanazotakiwa
kulipa Mamlaka ya Mapato, kodi ya Insuarence, kodi ya pikipiki
(motavehecle), na kodi ya fire dinstungsher pamoja na kodi ya maegesho ya
pikipiki zao ambazo zote hizo ni vigumu kulipika kulingana na kipato chao.
Mwenyekiti wa waendesha bodaboda hao Wilaya ya Tanga, Daudy
Bilaly, amewataka madereva wenzake kuwa na umoja na mshikamano ili kuweza kuktatua
kero zao kwa umoja.
Akizungumza katika kikao hicho, kamanda wa usalama
barabarani Mkoa wa Tanga, Abdi Issango, aliwataka madereva wa pikipiki kuacha
mtindo ulioibuka wa kupakiza abiria zaidi ya mmoja na kusema kuwa msako wa
kukomesha tabia hiyo utaanza mara moja.
No comments:
Post a Comment