Tafiti zinaonyesha
kuwa takribani Hekta milioni 44 za misitu hupotea kila mwaka nchini, ambayo ni
hasara inayotokana na uharibifu wa ardhi, hasara hii kubwa kwa Taifa hususan kwa
mkulima aliyoko kijijini inahitaji matumizi endelevu ya ardhi yatakayosaidia
kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na kuongoa ardhi iliyoharibika.
Hayo yameelezwa leo na Dk. Julius Ningu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais alipokuwa akizungumza, mjini Bagamoyo katika kikao cha wadau wa kamati ya taaluma ya utekelezaji wa masuala ya mradi chini ya mkataba wa umoja wa mataifa wa kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame ambapo Tanzania ni mwanachama.
Dkt Ningu aliwaeleza wana taaluma hao kuwa, Matumizi endelevu ya ardhi yanasaidia kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na kuongoa ardhi iliyoharibika.
Akitolea mfano wa baadhi ya maeneo nchini ambayo kwa kiasi kikubwa yana tatizo la kuenea kwa hali ya jangwa kama vile Maeneo ya katikati ya nchi ikiwa ni pamoja na mikoa ya Dodoma na Singida; na baadhi ya sehemu katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Iringa, Manyara na Dkt. Ningu ameeleza kuwa, maeneo haya yanakabiliwa na upungufu mkubwa wa misitu na kuongeza kuwa, Kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kunasababisha kupungua kwa uwezo wa ardhi kuzalisha mazao na upungufu wa malisho ambao pia hupunguza uzalishaji kwa upande wa mifugo.
Aidha aliwasisitizia wadau kuwa, Usimamizi Endelevu wa ardhi ni muhimu sana kuigwa na kutumika katika maeneo mengine nchini na kuwafahamisha kuwa taarifa muhimu watakazozipata katika mkutano huu, wazitumie kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili kwa sasa na vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment