JAMII imetakiwa
kuwasaidia, kuwajali na kuwatahamini
watoto yatima na walemavu kwani wanahaki ya kuishi kama watoto wengine.
Hayo
ameyasema mshauri wa mradi wa kitaalum kutoka nchini Finland Tero Tapani wakati akizungumza katika sherehe
ya watoto yatima na walemavu ambayo imefanyika katika ukumbi wa mkutano YDCP
Jijini Tanga.
Aidha
mtu ambaye atamthamini mtoto mlemavu na kumtunza atakuwa amefanya jambo la
Baraka mbele za Mungu na mbele za wanadamu.
Naye
Mratibu wa kituo hicho William Henry amesema kuwa lengo la kuadhimisha sikukuu
hiyo ya watoto kila mwaka ni kuwaweka watoto hao pamoja ili nao wao wajisikie
vizuri kama watoto wengine.
Kwa
upande wake mgeni rasmi ambaye ni Mch. Wa kanisa la FPCT Free Pentekoste Of
Tanzania Ayubu Kuminambili ambaye alimwakilisha makamu Askofu wa Taifa wa
kanisa Stivie Mulenga amesema kuwa amdharauliye wenzake atenda dhambi bali
amhurumiaye mwenzake ana heri,hivyo ni vyema kuwapenda watoto walemavu na kuwatunza
kwani Mungu amewaumba kwa makusudi maalum.
No comments:
Post a Comment