HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 2 December 2014

MICHEZO:MANDAWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU MWEZI NOVEMER..!!

MANDAWA AMBWAGA OWINO TUZO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU NOVEMBA
MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar ya Bukoba, Rashid Mandawa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja.
Mandawa ambaye kwa mwezi huo alichuana kwa karibu na mshambuliaji Fulgence Maganda wa Mgambo Shooting ya Tanga na Nahodha wa Simba, Joseph Owino atakabidhiwa zawadi yake na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya Vodacom.
Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo inatarajiwa kufanyika wakati wa mechi ya raundi ya nane ya ligi hiyo kati ya Simba na Kagera Sugar itakayochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
KOZI YA UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA SASA MACHI
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limesogeza mbele kozi ya ukufunzi ya utawala wa mpira wa miguu iliyokuwa ifanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa FIFA, kozi hiyo sasa itafanyika Machi mwakani katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
TFF imepokea maombi ya zaidi ya washiriki 40 kwa ajili ya kozi hiyo itakayoshirikisha washiriki 30. Kutokana na maombi kuzidi idadi ya nafasi zilizopo, FIFA itafanya mchujo wa washiriki.


MIKOA MITANO YATAKIWA KUWASILISHA USAJILI COPA 2014
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitaka mikoa mitano kuwasilisha usajili wa wachezaji wake kwa ajili ya mashindano ya Taifa ya Copa Coca-Cola 2014 kabla ya Desemba 5 mwaka huu.
Mikoa hiyo ambayo haijawasilisha usajili wake hadi sasa kwa ajili ya michuano hiyo inayoanza Desemba 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam ni Arusha, Dodoma, Katavi, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Mjini Magharibi na Simiyu.
Kwa mujibu wa Kamati ya Mashindano ya michuano hiyo, mkoa ambao hautawasilisha usajili wake kwa ajili ya uhakiki wa umri wa wachezaji utakaonza Desemba 10 mwaka huu utaondolewa katika fainali hizo zitakazomalizika Desemba 20 mwaka huu.

Wachezaji watakaobainika kuzidi umri hawataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 15. Kwa mujibu wa Kanuni ya 29 ya michuano kuhusu idadi ya wachezaji, kila timu inatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 20 na wasiopungua 16.
Hivyo, kila timu inatakiwa kuhakikisha inakuwa na idadi hiyo ya wachezaji, kwani kikanuni wakipungua 16 itaondolewa kwenye mashindano.
Timu 16 kwa upande wa wavulana zitashiriki katika fainali hizo wakati kwa upande wa wasichana ni timu nane. Mikoa iliyoingiza timu za wasichana kwenye fainali hizo ni Arusha, Dodoma, Ilala, Kinondoni, Mbeya, Mwanza, Temeke na Zanzibar.
TWIGA STARS KUINGIA KAMBINI MWAKANI
TIMU ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ inatarajiwa kuanza kambi Januari mwakani kwa maandalizi ya michuano ya Afrika ‘All African Games’.
Twiga Stars inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Machi mwakani dhidi ya Zambia. Ni muda mrefu kikosi hicho hakijaandaliwa programu za mechi za kirafiki kwa ajili ya kuwaweka sawa.
Hivi karibuni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alitangaza kwamba timu ya Taifa ya Vijana haitashiriki michuano ya Olimpiki, hivyo fedha ambazo zilikuwa zitumike katika program hiyo, zitakwenda kwa timu ya taifa ya wanawake kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika.

Akizungumza na gazeti hili jana kuhusu programu za Twiga Stars, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi alisema kabla ya kuanza kushiriki michuano hiyo kocha amependekeza kikosi hicho kicheze mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe kwa ajili ya kujiweka vizuri.
Akizungumzia mpango wa kuinua soka la wanawake nchi nzima, Madadi alisema wanakusudia kuanzisha ligi ya wanawake lakini kwanza kuhamasisha kila mkoa kuwa na timu ili kuwa rahisi kuandaa mashindano hayo.

Alisema ili mpango huo ufanikiwe wanahitaji kuungwa mkono na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali na Mitaa (TAMISEMI).

Madadi alisema pia kuwa kuna miradi mingine ya kuendeleza soka la wanawake katika rika zote za umri ambapo tayari wamepeleka mradi huo Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa ajili ya kuona kama watawaunga mkono kifedha.
POLISI MORO NA MWADUI FC ZAMTOLEA MACHO KINDA MIRAJI ADAM LA SIMBA
Timu Polisi ya Morogoro na Mwadui FC ya Shinyanga zimewasilisha barua kumuomba beki wa pembeni Miraj Adam wa Simba SC kwa mkopo baada ya kushushwa Simba B.
Polisi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inapambana na Mwadui FC, inayopigania kupanda Ligi Kuu pia kuwania huduma za beki huyo aliyetokea timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi.
Mwadui wanaamini wanaweza kumpata kwa urahisi beki huyo kwa sababu ya mahusiano mazuri ya kocha wao, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na klabu ya Simba SC.
Lakini Polisi nayo inaamini inaweza kumpata kwa urahisi beki huyo wa kulia, Miraj, kwa sababu inacheza Ligi Kuu kwa sasa na Morogoro si mbali sana na Dar es Salaam anakoishi mchezaji huyo.
Kwa sasa, Miraj ameshushwa kikosi cha pili baada ya mechi saba za awali za Ligi Kuu, lakini Simba SC bado haijaamua kumtoa kwa mkopo hadi hapo itakapofanikisha kusajili mchezaji mwingine wa nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment