HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 2 December 2014

WAZAZI TANGA WAASWA KUHUSIKA KATIKA KUIBUA VIPAJI VYA WATOTO.



WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kushirikiana na walimu wa shule za awali  ili kuibua, na kuendeleza na vipaji na vipawa vya watoto wao.

Rai hiyo imetolewa na katibu mkuu wa chama cha wanajombe waishio Jijini Tanga (uwanjota) bwana Bernard Goliama kwenye sherehe za kuwaaga watoto wa shule awali ya Front Runner Day Care Centre iliyofanyika hivi karibuni  kwenye hoteli ya Nyinda iliyopo eneo la Bombo jijini Tanga.
Amesema kila mzazi na mlenzi nchini awajibike kuendeleza watoto kwa ngazi ya elimu ya awali  ili Tanzania iwe na wataalam wengi  waliyo na misingi imara ya masomo  yenye faida kwa manufaa ya  sasa na baadaye.
Hata hivyo Goliama hakusita kuwapongeza na kudhamini walimu na uongozi wa shule ya Front Runner Day Care Centre kwa jitihada ya kutoa  elimu ya watoto hao ambao ni zaidi ya watoto 25 wamemaliza elimu hiyo ya awali kwa huu 2014.
Sambamba na hayo watoto wa shule hiyo kwa kupitia risala waliyosoma wamewaomba  wadau wa elimu kusaidiana na uongozi wa shule kuwajengea uzio wa shule hiyo ili waweze kusoma na kucheza kwa utulivu , furaha na amani.

No comments:

Post a Comment