HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Wednesday, 3 December 2014

MICHEZO LEO: MOMBEKI ATUA RUVU, THE EXPRESS YA UGANDA KUZIPIMA SIMBA, YANGA



RUVU SHOOTING YAMNASA MOMBEKI
Klabu ya Ruvu Shooting ya Pwani, imeamua kumwaga nyota watano kwa mpigo katika harakati za kutafuta mastraika, safu ambayo imewasumbua kwa muda mrefu tangu kuondoka kwa Elias Maguli aliyetimkia Simba.

Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire, alisema nyota hao tayari wameanza majaribio tangu juzi Jumatatu ambapo wataangalia wenye uwezo zaidi kabla ya kuwapa saini.
Bwire amesema kuwa wameamua kuvalia njuga safu hiyo kwani ndiyo iliyoonyesha matatizo zaidi katika mechi saba za mzunguko wa kwanza.
Imeelezwa kuwa  mshambuliaji wa zamani wa Simba, Betram Mwombeki amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Ruvu Shooting.
Mwombeki ambaye aliachwa na Simba na baadaye kwenda Oman kufanya majaribio ambako imeelezwa hakufuzu, amesaini kuichezea Ruvu Shooting leo.
Maana yake, mshambuliaji huyo ataanza kuonekana kwenye mechi za Ligi Kuu Bara zitakazoanza tena Desemba 26, mwaka huu.

THE EXPRESS YA UGANDA KUZIPIMA SIMBA, YANGA KABLA YA MTANI JEMBE

TIMU ya soka ya The Express ya Uganda inatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa na timu za Simba na Yanga.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mratibu wa mechi hizo, George Wakuganda amesema kuwa baada ya mashabiki wa soka nchini kukaa muda mrefu bila kushuhudia mechi, wameona ni vyema kuileta timu hiyo ili kucheza na vigogo hivyo vya soka nchini.Amesema The Express wataanza kucheza na Simba Ijumaa na kisha Yanga Jumamosi mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Amesema ni fursa nzuri kwa makocha wa pande zote mbili kuangalia upungufu kwenye vikosi vyao kabla ya mechi yao ya Desemba 13.Wakuganda amesema ameshafanya mazungumzo na pande zote mbili za uongozi wa Simba na Yanga na wote wamekubali kucheza mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa.
Kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo Simba ilikuwa ikifanya mazungumzo na mchezaji Dan Ssemkuruma ambaye anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ajili ya kumalizana na klabu hiyo kutoka mitaa ya Msimbazi.Kwa wachezaji wa ndani Simba inaonyatia kwa sasa ni Nurdin Choma wa Prisons ya Mbeya anayecheza nafasi ya beki wa kati na beki wa kulia Salum Kimenya wa Prisons pia. Simba pia inataka kuwabomoa Mbeya City kwa kumsajili kiungo mshambuliaji Deus Kaseke.
Endapo Simba itamalizana na wachezaji hao, Ijumaa wanaweza kuonekana uwanjani. Yanga itatumia nafasi hiyo kumtambulisha kiungo wao mpya Mbrazil Emerson De Oliveira Neves Roque.


AZAM FC SASA KUSAJILI MUIVORY COAST MWINGINE
KLABU ya Azam FC imeonekana kunogewa na wachezaji wa Ivory Coast na sasa ina mpango wa kumsajili Sanaly Bamba kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho chenye makazi yake Chamanzi.
Tayari Azam ina wachezaji watatu wa Ivory Coast ambao ni Pascal Wawa aliyekuwa akikipiga El Mereikh ya Jamhuri ya Sudan, Kipre Tchetche na Kipre Bolou. Mchezaji huyo tayari yupo nchini kwa takriban wiki mbili akifanya mazoezi. Alitokea Nigeria alipokuwa akicheza soka.

Meneja wa Azam FC Jemedari Said alisema Bamba atasajiliwa iwapo Kocha Mkuu wa klabu hiyo Joseph Omong na msaidizi wake George Nsimbe ‘Best’ watakubali kiwango chake.
Alisema Nsimbe ndio kwanza ameanza kazi tangu juzi hivyo anahitaji kumwona mchezaji huyo kisha kuungana na Omong katika maamuzi ya pamoja.
Wakati Nsimbe anatua nchini hivi karibuni alisema Uganda kuna wachezaji wengi wazuri wenye vipaji hivyo atatumia nafasi yake kuwasajili kwenye timu hiyo iweze kufanya vizuri.
Klabu hiyo ya Azam FC ilionesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Mali Mohamed Traore aliyekuwa akikipiga katika klabu ya El Mereikh lakini mpaka sasa haijawa wazi kama watamsajili ama la.
Azam inasajili kujiimarisha kutetea taji lake la Ligi Kuu, haina mwenendo mbaya kwenye ligi kwani inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 sawa na Yanga iliyo nafasi ya pili. Kinara wa ligi hiyo ni Mtibwa Sugar ikikaa kileleni kwa pointi 15.

No comments:

Post a Comment