| Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Hawa Gasia |
SERIKALI nchini imekili Uchaguzi
uliomalizika jana wa Serikali za Mitaa ulikuwa na Dosari katika baadhi ya
Maeneo mbalimbali nchini na kusema itawachukulia Hatua kali za Watendaji
Halmashauri Mbalimbali waliopelekea kuwepo na Dosari hizo.
Pia Licha ya kuwa na Dosari lakini
Badao Serikali imesema uchaguzi huo umefanikiwa kwa asilimia 98,Tofautisha na
Miaka mingine.
Hayo yemesemwa leo Jijini Dar Es Salaam
na Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi) Hawa Gasia wakati wa Mkutano na Waandishi ili
kuzungumzia uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa ambapo pamoja na Mambo Mengine
Waziri Gasia alikili kuwepo na Dosari kwenye Vituo mbalimbali vya kupiga kura
katika baadhi ya Kata,Vijiji,Mtaa au Vitongoji
Vilevele Waziri Gasia alisema Halmashauri na
Maeneo yenye Kasoro ambayo hayakufanya Uchaguzi,yatarudia uchaguzi huo ndani ya
Siku (7) kama kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinavyoelekeza.
Aidha,Waziri Gasia aliitaja Mikoa ambayo
Dosari zilijitokeza na kupelekea kuhailishwa kwa uchaguzi huo katika
baadhi ya Kata, vitongoji na Vijiji ni, Kilimanjaro ,
Manyara,Morogoro,Shinyanga,Simiyu,Kigoma,Mwanza,Tabora,Tanga,Mara,Rukwa,Dar Es Salaam,pmoja
na Mkoa wa Pwani.
Waziri Gasia aliongeza kuwa kwa ujumla
Halmashauri ambazo hazinadosari ni 145 kati 162 zilizofanya uchaguzi ambapo
Halmashauri tatu kati ya hizo hazikufanya Uchaguzi kabisa kutokana na
kucheleweshwa kwa Vifaa.
Hatahivyo Waziri Gasia aliziagiza Halmashauri
hizo uchaguzi kufanya haraka ndani ya siku 7 na vilevile Wizara hiyo ya
TAMISEMI itawachukuli hatua kali za watendaji waliopelekea Dosari hizo.
“Tumeitaka Mikoa Iwasilishe Taarifa
rasmi na kamiilifu kuhusu Kilichojitokeza katika Halmashauri hizo na
Wizara itachambua taarifa hizo ili kubaini wote waliosababisha kasoro
wachukuliwe hatua stahiki ikiwemo kusimamisha kazi,kukatwa mishahara,pamoja na
kufukuzwa kazi”alisema Waziri Gasia.
Waziri Gasia aliongeza kuwa licha ya uchaguzi
wa mwaka huu wa Serikali za Mitaa kuwepo na Changamoto mbalimbali lakini
serikali imefanikiwa uchaguzi huu kwa asilimia 98 tofautisha na miaka mingine.
No comments:
Post a Comment