MWADUI FC YA JULIO YAKAMILISHA USAJILI, YAMTWAA BEKI WA SIMBA
Katika hatua nyingine Mwadui FC imewatema wachezaji wawili wakongwe Salum Sued Kusi na Victor Costa.Kusi aliwahi kung'ara na Yanga pamoja na Mtibwa Sugar kama ilivyo kwa Costa aliyewahi kufanya vizuri na Mtibwa kabla ya kung'ara zaidi na Simba.
Imeripotiwa kuwa Mwadui FC pia imemnsa kiungo mwenye kasi Uhuru Selemani.Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwhelo 'Julio' amethibitisha kumtwaa Uhuru.
Klabu
hiyo pia imefanikiwa kumnasa beki Joram Mgeveke wa Simba.
Beki huyo anayekipiga katika kikosi cha Taifa Stars amejiunga na Mwadui FC jana kwa mkopo.Mwadui pia imemasajili Mohammed Mkweche.
Beki huyo anayekipiga katika kikosi cha Taifa Stars amejiunga na Mwadui FC jana kwa mkopo.Mwadui pia imemasajili Mohammed Mkweche.
EXCLUSIVE:...SIMBA YAFUNGA MKATABA NA BEKI KESSY WA MTIBWA SUGAR
Simba
imefunga usajili rasmi kwa kumsajili beki wa kulia, Ramadhani Kessy kutoka
Mtibwa Sugar.Kessy amejiunga na Simba jana baada ya kusaini mkataba wa kuichezea Simba kwa
miezi 18.Kessy amesaini mkataba huo mbele ya Meneja wake, Athumani Tippo pamoja
na Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu'.
Tetesi
zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni
30.
EXCLUSIVE; TAMBWE RASMI ASAINI YANGA.
Hayawi
Hayawi, Hatimaye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Amissi Tambwe
amesaini Yanga.Tambwe amejiunga na Yanga jana ikiwa ni dakika chache baada ya Simba kumtema.
Mbele ya Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Francis Kifukwe, Tambwe
ameanguka kuitumikia Yanga kwa mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment