
Miili ya watu wapatao 129 imepatikana kutoka Ziwa Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, baada ya feri kupinduka na kuzama mapema Ijumaa.
Waziri
wa Uchukuzi nchini humo Laurent Sumba Kahozi amesema msako unaendelea
kuwatafuta watu waliopotea katika ajali hiyo.
Wafanyakazi
wa uokoaji waliwapata abiria wakielea katika maji Jumapili, wakiwa katika
mapipa ya petroli na vifaa vingine.
Maboti
katika eneo hilo mara nyingi hujazaa abiria na mizigo kupita kiasi na ajali
kutokea ni jambo la kawaida
Habari
zinasema ajali kama hiyo ni za kawaida katika eneo hilo kutokana na boti kujaa
abiria na mzigo kupita kiasi.
Maboya
ya kujiokoa mara nyingi hayamo katika maboti hayo na watu wengi hawawezi
kuogelea.
Maafisa
katika jimbo la Katanga wamesema upepo mkali na kujaza abiria na mizigo kupita
kiasi kumesababisha boti MV Mutambala, kupinduka.
Wanawake
na watoto ni miongoni mwa watu waliokumbwa na ajali hiyo ambayo ilitokea mapema
Ijumaa asubuhi.
Taarifa
za awali zilisema watu 26 wamekufa katika ajali hiyo.
Idadi
ya watu walionusurika imetajwa kuwa watu 232, wengi wakiwa ni wanaume, amesema
waziri wa uchukuzi katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment